Friday 25 May 2018

Kipa Ujerumani Aendelea Kuwa Fiti Kombe la Dunia

Kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Manuel Neuer.

MUNICH, Ujerumani
KIPA wa Ujerumani Manuel Neuer yuko mbioni kuwa fiti kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia baada ya kupona maumivu ya mguu yaliyomuweka kando kwa karibu msimu mzima, alisema juzi kocha wa timu ya taifa Joachim Loew.

Akizungumza wakati wa kuanza kwa mazoezi ya timu hiyo katika kambi yao kaskanzini ya Italia, Loew alisema anauhakika kuwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye ni nahodha wa timu ya Ujerumani, sehemu ya timu iliyotwaa Kombela Dunia 2014, atacheza Urusi.

Neuer ambaye ni kipa wa Bayern Munich hajacheza soka tangu alipovunjika mfupa wa mguu wake Septemba mwaka jana, ambapo alihitaji kufanyiwa upasuaji na kumfanya kuwa katika wasiwasi wa kucheza fainali hizo.

"alifanya mazoezi wiki katika klabu ya Bayern, hapa anafanya mazoezi kamili na anaendelea kuwa fiti, “alisema Loew alipozungumza na waandishi wa habari.

"Tutaangalia mazoezi ya siku hadi siku. Ikiwa atakuwa fiti kwa asilimi 100 basi hakuna ubishi atakwenda Urusi kwa ajili ya fainali hizo, na kama kutakuwa na tatizo lolote, basi itabidi kuzungumza….”

Loew pia anatarajia kurejea kwa Jerome Boateng katika kikosi chake wiki hii wakati beki huyo wa kati akipona maumivu ya nyonga aliyoyapata mwezi uliopita.

"Kila kitu kinakwenda vizuri kama kilivyopangwa na wiki ijayo tunamtarajia kushirii katika mazoezi, “alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 58, ambaye mwezi huu ameongeza mkataba wake utakaompeleka hadi mwaka 2022.

Wajerumani wanajifua katika milima ya Alps nchini Italia kwa ajili ya maandalizi ya kutetea taji la Kombe la Dunia, huku Loew akiwapongeza wachezaji wake wakati wakiwa tayari kwa ajili ya kutetea taji lao.

"Hapa kuna hali nzuri sana, uwanja mzuri, hoteli nzuri sana, sehemu ya kuchezea iko katika hali nzuri sana, hivyo kila kitu kiko katika hali nzuri sana.”

Ujerumani itaaendelea kubaki Italia hadi Juni 5, siku moja baada ya siku ya mwisho ya kutangaza kikosi cha mwisho. Loew ina wachezaji 27 katika kambi hiyo huku wanne wakitarajiwa kupigwa `panga’.

Ujerumani itasafiri na kwenda kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki ugenini dhidi ya Austria huko Klagenfurt Juni 2 kabla hajarejea na kukukabliliana na Italia kabla haijarudi nyumbani kuikabili Saudi Arabia huko Leverkusen siku sita baadae, wako katika Kundi F pamoja na Sweden, Korea Kusini na Mexico.

No comments:

Post a Comment