Friday 25 May 2018

Misri Wajifua kwa Kombe la Dunia Urusi 2018

CAIRO, Misri
TIMU ya taifa ya Misri itacheza dhidi ya Kuwait kesho Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa kirafiki kati ya 15 itakayochezwa na timu hiyo ya Afrika iliyofuzu kucheza Kombe la Dunia itakayofanyika kuanzia Juni 14hadi Julai 15 nchini Urusi.

Timu za taifa ya Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia zinaliwakilisha bara ya Afrika katika Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi.

MIsri watamkosa mkali wao Mohamed Salah huko Kuwait City wakati akiichezea klabu yake ya Liverpool ambayo leo inacheza dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya leo.

Nyota mwingine wa Kombe la Dunia, Sadio Mane wa Senegal, naye pia atakuwa katika jezi ya Liverpool akijaribu kuizuia Real Madrid kutwaa taji lake la nne mfululizo la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Baada ya kucheza na Kuwait, kikosi hicho cha timu ya taifa ya Misri ambacho kinafundishwa na kocha wa Argentina Hector Cuper atakiongoza kwenda Ulaya kucheza na Colombia huko Milan na baadae Ubelgiji jijini Brussels.

Morocco, imerejea katika Kombe la Dunia baada ya miaka 20 ya kutokuwepo, itakwaana na timu ambazo hazijafuzu kwa Kombe la Dunia Ukraine na Slovakia katika jiji la Uswisi la Geneva kabla ya kukabiliana na Estonia huko Tallinn.

Nigeria ndio nchi pekee ya Afrika ambayo itacheza mchezo wa kujipima nguvu barani, ikiikaribisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huko Port Harcourt Jumatatu hii.

Timu hiyo ya 'Super Eagles' baadae itakabiliana na England kwenye Uwanja wa Wembley na Jamhuri ya Czech huko Austria kabla haijapanda ndege na kwenda Urusi, nchi ya kwanza ya Ulaya Mashariki kuandaa fainali za Kombe la Dunia.

Senegal, inashiriki kwa mara ya pili baada ya kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2002 na kutinga robo fainali, itacheza dhidi ya Luxembourg na Croatia kabla haijakutana na Korea Kusini bila wachezaji kwenye Uwanja wa Australia.

Tunisia, bila kushinda mechi 14 za Kombe la Dunia tangu ilipowafunga Mexico mwaka 1978, watakuwa ugenini wakicheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya Ureno kabla hawajakutana na Uturuki huko Uswisi na Hispania huko Urusi.

Nchi tani za Afrika zilizofuzu zinarejea mchezoni kwa mara ya kwanza tangu Machi wakati walipopata matokeo tofauti tofauti walipocheza mechi za kirafiki.

Misri ilichapwa 2-1 na Ureno baada ya Cristiano Ronaldo kufunga mara mbili katika muda wa majeruhi na timu hiyo iliyobadilika sana ilijikuta ikifungwa 1-0 na Ugiriki.

Morocco iliwafunga Serbia 2-1 huko Italia na kurejea nyumbani ambako walishinda 2-0 dhidi ya Uzbekistan.

No comments:

Post a Comment