Tuesday 1 May 2018

Serena Williams Kupanda Chati Wimbledon 2018


NEW YORK, Marekani
BINGWA mara saba Serena Williams bado anaweza kuwa namba moja katika mashindano ya Wimbledon mwaka huu, hata kama Mmarekani huyo hajarejea ndani ya nafasi 32 bora duniani kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

Williams, 36, aliporomoka kwa viwango hadi kufikia nafasi ya 449 duniani tangu alipojifungua mwaka jana.

Anaamini wachezaji wanaotoka kujifungua wanatakiwa kulindwa katika upangaji wa ratiba pamoja nakulindwa katika viwango.

Richard Lewis, mtendaji mkuu wa klabu ziote za England, alisema kuwa huo ni “uamuzi mkubwa”.

Lewis alisema kuwa anfikiri hilo klitatokea kwa Williams kwani anaweza kupangwa katika mashindano hayo, licha ya kuwa nje ya 32 bora, mashindano hayo yataanza Julai 2.

Hatahivyo, klabu baadae ilitoa taarifa kuwa ni ubaguzi kuwapanga wachezaji katika mashindano kwa kuzingatia viwango vyao.

Mkutano wa upangaji ratiba unatarajia kufanyika Juni 26.

Williams, ambaye alijifungua mtoto wakike anayeitwa Alexis Olympia Ohanian Jr Septemba, amecheza mechi nne za mchezaji mmoja mmoja tangu aliporejea katika mchezo huo, ambapo alifikia katika hatua ya 32 bora katika mashindano ya Indian Wells kabla hajapoteza kwa dada yake Venus na baadae alitolewa na nyota Mjapan anayeinukia Naomi Osaka katika raundi ya kwanza huko Miami.

No comments:

Post a Comment