Friday 25 May 2018

Mashabiki England Kufurika Kombe la Dunia Urusi

Nahodha wa England, Harry Kane.

MOSCOW, Urusi
HADI mashabiki 10,000 wa soka kutoka England wanatarajia kutua nchini hapa mwezi ujao ili kuiunga mkono timu yao itakapokuwa ikicheza mechi za Kombe la Dunia mwaka huu, amesema msemaji wa Ubalozo wa Uingereza mjini hapa juzi.

Msemaji huyo akizungumza na Shirika la Habari la Urusi, Tass, alisema kuwa wanatarajia raia karibu raia 10,000 kutoka Uingereza kutembelea Urusi mwaka huu kwa ajili ya kuja kushuhudia fainali za Kombe la Dunia.

“Tunatarajia karibu wapenzi wa soka 10,000 kutoka Uingereza kutembelea Urusi mwaka huu kuja kushuhudia fainali za Kombe la Dunia na kuja kufurahia uhusiano mzuri kati ya Uingereza na Urusi kabla ya Kombe la Dunia kwa miaka miwili sasa.

"Ofisa wa usalama Mark Roberts (ambaye anashughulikia sera za soka) alitembelea mara mbili nchini Urusi mwaka jana, “alisema. “Msafara wa Polisi wa Uingereza walifanya kazi wakati wa mechi za Kombe la Shirikisho la Dunia kwa  Klabu Julai mwaka jana.

Gazeti la Uingereza la Daily Star wiki hii liliandika ripoti kuwa mashabiki wa soka wa England watakuwa wakitafuta kitu huko Urusi wakati wa Kombe la Dunia na hilo litakuwa kama Vita ya Tatu ya Dunia, Nne, Tano, Sita na Saba.”

Vurugu kadhaa ziliripotiwa kati ya mashabiki wa soka wakati wa mashindano ya Kombe la Uefa huko Ufaransa kati ya Juni 10 na Julai 10, 2016. Mpambano mkubwa uliowahi kuibuka kati ya mashabiki wa Urusi na Waingereza wakati ikielekea mechi ya Juni 11 huko Marseilles.

Fainali za Kombe la Dunia 2018 zinatarajia kuanza Juni 14 hadi Julai 15 nchini Urusi huku mechi ya ufunguzi ikitarajiwa kupigwa mjini hapa.

Urusi imechagua miji 11 kuchezwa fainali hizo, ambayo ni Moscow, St. Petersburg, Sochi, Kazan, Saransk, Kaliningrad, Volgograd, Rostov-on-Don, Nizhny Novgorod, Yekaterinburg na Samara.

No comments:

Post a Comment