Tuesday 1 May 2018

Zidane Aaanza Nyodo, Real Ikitinga Fainali Ulaya


MADRID, Hispania
ZINEDINE Zidane anasema kuwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya “ni vinasaba vya Real Madrid” baada ya kikosi chake kutinga kwa mara ya nne fainali ya mashindano hayo katika kipindi cha miaka mitano.

Real ilipata nafasi hiyo ya kucheza fainali ikisaka kushinda kwa mara ya tatu mfululizo taji hilo baada ya Karim Benzema kufunga mara mbili na kuwawezesha mabingwa hao watetezi kutoka sare ya 2-2 na kupata ushindi wa jumla wa 4-3 dhidi ya Wajerumani Bayern Munich.

Real Madrid tayari imeshuhudia wapinzani wao wakubwa Barcelona wakitwaa taji la La Liga ndhini Hispania msimu huu, lakini Zidane anasema mashindano hayo makubwa Ulaya mara nyingi timu yake inafanya vizuri, ambapo imeshatwaa taji hilo mara 12.

"Ni vinasaba vya klabu yetu. Kamwe hatuachi kupambana hadi katika dakika ya mwisho, kama walivyofanya Bayern usiku huu.”

Zidane alisema Benzema alikuwa zaidi ya kuanza katika mchezo huo baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa alitolewa katika kipindi cha kwanza katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliofanyika Jinini Munich.

"alistahili kufunga, alifanya kazi kwa bidii na kamwe huwa hana tabia ya kutojituma.

"Mchezo wake mara zote huwa ni sawa na amekuwa mchezaji mwenye msaada mkubwa ketu.”
Baada ya kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza nchini Ujerumani, Bayern Munich walikuwa wakihitaji ushindi katika mchezo huo wa marudiano uliofanyika kwenye Uwanja wa Bernabeu ili kutinga fainali lakini walijikuta wakimaliza mchezo huo kwa sare ya 2-2 na kupata ushindi wa jumla wa mabao4-3.

Joshua Kimmich aliifungia Bayern mapema kwa mkwaju wa umbali wa meta sita, kabla Karim Benzema hajafunga kwa kichwa akiisawazishia Real Madrid akiunganisha wavuni krosi ya Marcelo dakika nane baadae.

No comments:

Post a Comment