Sunday 13 May 2018

Liverpool Yashinda 4-0, Chelsea Yachapwa 3-0 EPL

Mohamed Salah

LONDON, England
MSIMU wa mwaka 2017/18 wa Ligi Kuu ya England ulimalizika jana kwa kishindi huku timu zingine zikicheka na zingine kulia kutokana na matokeo waliyoyapata.

Livepool ilitoka meno nne baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion, huku Chelsea ikipokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa New Castle United.

Ushindi huo umeifanya Liverpool kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu ujao, huku Chelsea akiikosa nafasi hiyo na kuambulia ile ya Ligi ya Ulaya msimu ujao.

Katika mchezo mwingine uliofanyika kwenye Uwanja wa Liberty, Swansea City ilijikuta ikilambwa mabao 2-1 dhidi ya Stoke City, huku Crystal Palace ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Brom.

Katike mchezo mwingine, kwenye Uwanja wa Turf Moor, Burnley ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa AFC Bournemouth huku Huddersfield Town ikichapwa 1-0 dhidi ya Arsenal na Manchester United wakiikandamiza Watford kwa bao 1-0.

Kwenye Uwanja wa St. Mary, Southampton ilichapwa bao 1-0 na mabingwa wapya Manchester City, ambao walifikisha bao la 100 na kuweka historia huku Tottenham Hotspur ikishinda 5-4 dhidi ya Leicester City.

No comments:

Post a Comment