Saturday, 22 July 2017

Kilimanjaro International Airport Marathon yaja


Na Cosmas Mlekani
MBIO kubwa zaidi za marathoni zinatarajia kufanyika Moshi Novemba 19 mwaka huu, ambazo zitajulikana kama Kilimanjaro International Airport  Marathoni, imeelezwa.

Mbali na kutarajia kushirikisha wanariadha wengi tena nyota kutoka ndani nan je ya Tanzania, mbio hizo zitakuwa zinaongoza kwa zawadi kubwa, ambao mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha sh milioni 7 ikiwa ni zawadi kubwa zaidi kuwahi kutolewa katika mbio za marathon hapa nchini.
Mkurugenzi wa Mbio hizo, Amini Kimaro akizungumza leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa mbio hizo, ambazo zinaandaliwa na kudhaminiwa na Kilimanjaro Airports Development Company (Kadco) na kusimamiwa na wataalam wa riadha, Amini Kimaro alisema mbio hizo zitaendeshwa kwa utaalam mkubwa.

Kimaro alisema kuwa mshndi wa pili wa mbio hizo za kilometa 42 ataondoka na kitita cha sh milioni 5 huku watatu atakabidhiwa kitita cha sh milioni 4 wakati mshindi wanne atapewa sh milioni 2.5 huku yule watano atabeba sh milioni 2.

Alisema kuwa zawadi za washindi watazitoa hadi kwa mshindi wa 10, ambaye ataondoka na kitita cha sh 500,000.
Mkurugenzi msaidizi wa mbio, Kunda Ndosi.
Mbio za Kilimanjaro Marathon ndizo awali zilikuwa zikichukuliwa kama mbio kubwa zenye zawadi kubwa, ambazo mshindi wa kwanza wa kilometa 42 anaondoka n ash milioni 4 wakati mshindi wa pili anapata sh milioni 2, watatu sh milioni 1, wanne 900,000, watano 600.000 wakati wa 10 ni sh 200,000.

Kwa upande wa mbio za nusu marathon au kilometa 21, zile za Kilimanjaro International Airort wenyewe mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha sh milioni 4 wakati Kilimanjaro Marathon wanatoa sh milioni 2 tu.
Mbio za Kilimanjaro International Airport zitatoa zawadi za fedha taslimu hata kwa wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za kilometa tano, mbio za Kilimanjaro Marathon zenyewe hutoa zawadi za saa na vitu vingine vinavyotolewa na wadhamini wa mbio hizo za kilometa tano.

Hakuna ubishi kuwa zawadi za washindi wa mbio hizo ni nono kweli ukilinganisha na zingine zote zinazofanyika hapa nchini katika vipindi tofauti tofauti vya mwaka.

Mbali na ukubwa wa mbio hizo, pia zitakuwa ni za kipekee kwani zitaanzia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kumalizikia katika maeneo hayo hayo.

Mbio hizi zitajumuisha zile za full marathon, yaani kilometa 42, nusu marathon yaani za kilometa 21 na zile za kilometa tano, ambazo wengine wanaziita mbio za kujifurahisha na hazina zawadi.

Hatahivyo, waandaaji wa mbio hizo za kimataifa za Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro, wenyewe watatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi watano, ambao watapata sh 500,000, 300,000, 250,000, 225,000 na 200,000.

Kimaro anasema kuwa wameamua kutoa zawadi nono ili kuvuta nyota wengi wa riadha hapa nchini na nje ya mipaka yetu ili kuzifanya ziwe kubwa zaidi.

Anasema kuna viwanja kadhaa vya ndege duniani vimekuwa vikiandaa mbio ili kuvuta watalii na watu wengine kama vile Dubai Marathon na Helsink nchini Finland.
Anasema mshindi wa pili ataondoka na kitita cha sh milioni 5, wakati wa tatu atapewa sh milioni 4,  huku yule wa nne atapewa sh milioni 2.5, watano sh milioni 2 na wa sita sh milioni 1.

Mshindi wa saba ataondoka na sh 800,000 wakati yule wa tisa atapata 700,000 wa tisa na 10 atapata sh 600,000 na 500,000.

MBIO MPYA ZA WANAFUNZI
Hii ni mara ya kwanza kwa waandaaji wa mbio kuwakumbuka wanafunzi, ambapo kutakuwa na mbio maalum za wanafunzi za kilometa 21, ambapo wanafunzi watatumia fedha za ushindi kulipia ada zao.

Mbali na kuwashindanisha wanafunzi, pia mbio hizo za nusu marathoni zitashirikisha wanariadha wa kawaida ambao nao watakuwa na zawadi zao.

Zwaadi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambao watashindana katika kilometa 21 zikuwa ni sh milioni 4 kwa mshindi wa kwanza wakati mshindi wa pili ataondoka sh milioni 3 wakati mshindi wa tatu atapata milioni 2.5.

Kimaro ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Riadha Wilaya ya Hai na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro alisema wanafunzi watatumia fedha hizo kwa ajili ya kulipia ada ya vyuo.

“Mbio za nusu marathoni ziko pande mbili, upande mmoja zinashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu ambao zawadi hizo za washindi zitawawezesha kulipia ada zao za vyuo, “alisema Kimaro.

3 comments: