Saturday, 22 July 2017

Stars yatoka sare na Rwanda, yatupwa nje Chan

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas.

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imetolewa katika kinyang’anyiro cha kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) baada ya kutoka suluhu na Rwanda katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amahoro nchini Rwanda.

Taifa Stars imeondolewa kwa faida ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya 1-1 na Rwanda katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na hivyo Stars ilikuwa ikihitaji angalau ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia bao 2-2.


Katika mchezo huo wa leo timu zote zilikosa mabao mengi baada ya kushindwa kutumia vizuri nafasi walizoata.

Kikosi cha Taifa Stars: 

1. Aishi Manula
2. Boniphace Maganga
3. Gadiel Michael
4. Erasto Nyoni
5. Salim Mbonde
6. Himid Mao
7. Simon Msuva
8. Mzamiru Yassin
9. John Bocco
10. Raphael Daudi
11. Shiza Kichuya

Kikosi cha akiba

12. Said Mohamed
13. Hassan Kessy
14. Nurdin Chona
15. Salimin Hoza
16. Said Ndemla
17. Joseph Mahundi
18. Stamili Mbonde

No comments:

Post a Comment