Sunday, 16 July 2017

Mourinho akata tamaa kumsajili nyota Ronaldo

 
MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho amebwaga manyanga kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid.

BBC Sport ilirioti Juni kuea Ronaldo alikuwa tayari kuondoka baada ya kutuhumiwa kukwea kulipa kodi na anataka kuondoka Hispania.

Kurejea Man United, ambako aliondoka wakati huo kwa ada iliyokjwa rekodi ya dunia ya pauni milioni 80 mwaka 2009, ilitajwa kama moja ya sehemu anayoweza kutua.

Hatahivyo, alioulizwa kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kurejea Man United, Mourinho alisema hilo haliwezi kutokea kutokana na ugumu wa kiuchumi wa kukamilisha uhamisho huo.

Mourinho alipoulizwa kumsajili nahodha wa Ureno Ronaldo Ronaldo baada ya timu yake kuifunga LA Galaxy 5-2 katika mchezo wa kwanza wa maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu mpya katika ziara ya Marekani leo Jumapili.

"Kamwe siwezi kuruhusu klabu yangu kupoteza muda kwa kitu ambacho hakiwezekani.
"Ronaldo ni mchezaji mzuri kwa klabu yake. Hatuna sababu ya kutufanya kufikiria kama Ronaldo kama anaweza kuondoka.”

Mourinho aliongeza kuwa aamini kuwa hakuna mchezaji mwingine wa Real Madrid, mshambulia Alvaro Morata, huenda akaishia Old Trafford.

"Ni aibu, " alisema.

No comments:

Post a Comment