Tuesday, 30 May 2017

Viongozi wapya Tava kupatikana Julai 8 Moshi

Makamu mwenyekiti wa Tava, Muharami Mchume.
Na Mwandishi Wetu
UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (Tava) umepangwa kufanyika Julai 8 mjini Moshi.

Kamati ya Utendaji ya Tava ilikutana juzi na kumalizika kikao chao usiku, ambapo walikubaliana kuwa uchaguzi huo ufanyike Moshi tarehe hiyo.

Makamu mwenyekiti wa Tava, Muharami Mchume alisema juzi kuwa, mikoa imetakiwa kufanya chaguzi zao mapema kabla ya huo wa taifa.

Alisema kuwa mikoa ambayo haijafanya chaguzi zao na kusajiliwa, kamwe haitaruhusiwa kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa Tava.

Alizitaja nafasi zigakazogombewa kuwa ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti wa kwanza anashughuliwa mipango na maendeleo, makamu wa pili anashughulikia fedha na utawala, katibu mkuu na katibu msaidizi.

Nafasi zingine ni zile za mwenyekiti wa kamisheni ya wavu wa ufukweni, Maendeleo ya Mikoa, kamiosheni ya Makocha, Waamuzi pamoja na ile ya Wanawake na Watoto.

Mchume alisema kuwa uchaguzi huo utasimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na tayari fomu za uongozi zimeanza kutolewa kwa wale wanaotaka kuwania nafasi hizo.


Wale wanaotaka kugombea nafasi za juu, watanunua fomu kwa sh 100,000 wakati viongozi wa kamishneni kila fomu itauzwa sh 50,000.

No comments:

Post a Comment