Monday 8 May 2017

Bunge Sports Club yaitambia NMB

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akimkabidhi kikombe Naodha wa timu ya Bunge Sports Club ambaye ni Mbunge wa Mbiga, Sixtus Mapunda baada ya timu hiyo kuifunga NMB Magoli 2-0  katika mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Timu ya Bunge Sports Club inayojumuisha timu ya mpira wa miguu, mpira wa pete na kikapu imeibuka washindi na kunyakua vikombe vitatu katika bonanza lililozikutanisha timu ya Bunge na timu ya benki za NMB.

Timu ya kwanza ya Bunge kushinda kikombe ilikuwa timu ya mpira wa pete ambayo iliifunga timu ya pete ya NMB magoli 19-2, ikifuatiwa na timu ya mpira wa kikapu kwa wanaume ambayo iliwafunga wapinzani wao timu ya mpira wa kikapu ya NMB kwa jumla ya vikapu 37-28.

Kikombe cha tatu kwa timu ya Bunge kilipatikana kwa timu ya mpira wa miguu, ambayo iliwafunga NMB mabao  2-0 na hivyo kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote ambao timu hizo zimekutana.


Timu ya Bunge Sports Club na NMB Sports Club zimekuwa zikikutana kucheza michezo mbalimbali zikiwa na lengo la kuboresha uhusiano baina ya Bunge na NMB, ambapo kwa mwaka huu bonanza hilo limefanyika katika Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment