Monday, 8 May 2017

Wavu Dar es Salaam waendelea kushika kasi

Wachezaji wa timu ya Jeshi Stars (kulia) wakipambana na wenzao wa Kinyerezi katika mchezo uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
LIGI ya Mpira wa wavu mkoa wa Dar es Salaam iliendelea tena jana Jumapili kwa michezo mitano kwenye Uwanja wa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.

Katika mechi za asubuhi, Makongo Wanawake iliifunga JKT kwa seti 3-0 ,huku timu ya wanaume ya Makongo iliilaza Victory kwa seti 3-0 .
Jeshi wanaume ambao wamezidi kujiimarisha katika msimamo wa ligi kwa upande wanaume, iliwafunga Kinyerezi kwa seti 3-0, Polisi Marine  ikapoteza kwa kufungwa na JKT kwa seti 3-2.
IP Sports Club ikaishinda Mjimwema kwa seti 3-1.

Katika mechi zingine zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Ndani asubuhi, Chui waliifunga IP Sports kwa seti 3-2, huku Jeshi Stars waliwatandika Victory kwa seti 3-0, ambapo Jeshi Stars walinufaika na ukubwa wa kikosi chao hicho.


Mjimwema waliifunga Kinyerezi kwa seti 3-0 huku JKT ikipata ushindi bila kushujka uwanjani baada ya wapinzani wao, Tanzania Prisons kutotokea uwanjani kwa wakati, katika mchezo mwingine, Jeshi Stars waliifunga vijana wa Makongo kwa seti 3-1.

1 comment:

  1. Safi sana napenda kutoa pongezi kwa timu zote na siku ya jumatano tarehe 10 ligi hiyo itaendelea uwanja wa ndani wa taifa kwa mchezo wa kwanza utakao anza saa tisa mchana kati ya TZ PRISNS vs MJIMWEMA wanawake na kuguatiwa na mechi nyingine kati ya TZ PRISONS vs VICTORY SPORTS wanaume.

    ReplyDelete