Monday, 8 May 2017

Juve wajiandaa kumaliza kazi Ulaya kesho

Wachezaji wa Juventus wakifurahia kwa mashabiki ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Monaco katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliofanyika Ufaransa wiki iliyopita. Timu hizo zinarudiana tena kesho Turin, Italia.
TURIN, Italia
SHUJAA aliyefunga mabao mawili Gonzalo Higuain amewataka wachezaji wenzake wa Juventus kugangamala wakati kesho watakaporudiana na Monaco katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Ufaransa, Juventus waliibuka na ushndi wa mabao 2-0, ambayo yalifungwa na Higuain na kuiweka timu hiyo katika nafasi nzuri ya kutinga fainali.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina alitengenezewa mpira na Dani Alves na kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 29 kabla ya kuihakikishia ushindi timu hiyo kwa bao la dakika 59 katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Stade Louis II.

Mabingwa hao wa Italia wako katika nafasi nzuri ya kuchea fainali ya mashindano hayo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Cardiff Juni 3 huku wakitarajiwa kukutana na timu yake yazamani ya Real Madrid.

"Kwa kweli ndoto tuliyokuwa nayo tangu Agosti mwaka jana ni kwenda Cardiff na tumebakisha hatua moja kuingia, “alisema Higuain, ambaye alipigiwa makofi na mashabiki huko Monaco.

Kwa sasa tayari ana mabao 31 katika msimu huu kufuatia uhamisho wake uliogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 98 akitokea Napoli, akiisaidia Juve kukaribia kutwaa mataji matatu.

Higuain, ambaye alicheza mechi saba bila ya kufunga bao katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya hatua ya mtoano, aliongeza: "Bado hatujashinda chochote hadi sasa. Wakati wote niko kimya. Najua kila mmoja ana imani naye.”

Juventus, ambayo itaikaribisha Monaco mjini hapa leo, sasa imecheza saa 10 bila ya kuruhusu bao katika mechi za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na kipa Gianluigi "Gigi" Buffon hajafungwa katika mechi zote tano za mtoano za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

"Katika kila mchezo nataka kuonesha kuwea nastahili kucheza katika kiwango hiki licha ya umri wangu. 

Nafanya kazi kwa bidii kila siku hadi pale nitakapoachia ngazi, “alisema Buffon.

Mara mbili kipa huyo akiwa golini timu yake ilifungwa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Buffon pia alimpongeza kocha Massimiliano Allegri kwa uamuzi wake wa kumleta Andrea Barzagli katika safu ya mabeki watatu, na kuzuia mashambulizi ya Monaco.


Wakati huohuo, mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya wenyewe watashuka dimbani kesho Jumatano kucheza na Atl├ętico Madrid baada ya ushindi wa awali wa mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment