Monday, 8 May 2017

BFT yatangaza timu ya taifa ya ndondi

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ndondi Tanzania (BFT) limetangaza mabondia 20 watakaounda timu za taifa za ndondi zitakazoshiriki mashindano ya Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, mabondia 15 wataunda timu ya ndondi ya wanaume wakati watano wataunda ile ya wanawake.

Kamati ya Ufundi ndio imeteua mabondia hao chini ya kocha David Yombayomba akishirikiana na makocha wa timu zote zilizoshiriki mashindano ya taifa yaliyofanyika hivi karibuni.

Mashindano ya taifa yalimalizika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Aprili 30 na kushirikisha mikoa michache tofauti na ilivyotarajiwa.

Timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Mkuu Mkenya, Benjamin Oyombi, ambapo itashiriki mashindano ya Afrika Brazzavile, Congo baadae mwezi huu.

Mabondia waliochaguliwa;-

Light Fly:   Herman Richard (Ngome)                                                                                                                                                              

Fly weight :      Ibrahim Aballah (Urafiki)      George Costantino (Ngome)

Bantam:    Ezra Paulo ( Ngome)

Light:   Ismail Galiatano (Ngome)  , King Lucas (Kigoma)

Lightwelter: Mohamed Juma (Ngome)  na  Kassim Seleman (Ngome)

Welter: Said Ramadhan (JKT) na Haruna Hussein (JKT)

Middle:  Seleman Kidunda

Light Heavy: Yusuph Changarawe

Heavy: Haruna swanga (Ngome)

Super Heavy: Mhina Morris (Ngome)   na  Alex Sitta (JKT)


Wakati wanawake ni Sara Andrew ( Ngome), Grace Joseph (JKT), Siwatu Eliuta (JKT), Sarafina James (JKT) na Aliskunda Jonas (Kigoma).

No comments:

Post a Comment