Tuesday 9 May 2017

SpotiPesa yamwaga Mil 50 Serengeti Boys

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa Kampuni Mpya ya kubeti ya SpotiPesa jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mikurugenzi wa Michezo nchini, Yusuph Singo na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SpotiPesa, Abbas Tarimba wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI mpya ya michezo ya kubahatisha ya Spoti Pesa ya Kenya imeipiga jeki timu ya taifa ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys, baada ya kutoa sh. Milioni 50.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SpotiPesa nchini, Abbas Tarimba aliahidi kutoa kiasi hicho cha fedha wakati wauzinduzi rasmi wa kampuni hiyo hapa nchini jijini Dar es Salaam jana.

Alisema kampuni yake imetoa fedha hizo ili kumfuta machozi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe ambaye usiku kucha juzi alisafiri kutoka Dodoma ili kuwahi uzinduzi huo.
Dk Mwakyembe alikuwa Dodoma, ambako juzi bajeti ya wizara yake ya mwaka 2016-17 ilipitishwa.
Serengeti Boys iko Gabon tayari kwa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, ambako itaanza kampeni zake kwa kucheza na mabuingwa watetezi Mali Mei 15.

Awali, akizungumza katika hafla hiyo Dk Mwakyembe alisema kuwa, Serikali iko pamoja na kampuni hizo na itatoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha inafikia malengo yake.
Alisema kuwa tayari Tanzania ina akina Mbwana Samatta 22 waliomo Serengeti Boys, ambapo aliwaeleza SpotiPesa kuwa hawatapata shida ya kusaka vipaji na kuviendeleza kwani tayari wako wengi.

Awali, Tarimba alisema kuwa kampuni hiyo mbayo ilianzishwa nchini Kenya mwaka 2014 na ina mataiwi jijini Nairobi na Liverpool nchini Uingereza na sasa jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa kampuni hiyo itakuwa miongoni mwa kampuni tano bora zitakazokuwa zikiingizia Serikali fedha nyingi kupitia kodi itakazolipa.


Baadhi ya wadau wengine wa soka waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, Makamu wa Rais wa Simba, Nyange Kaburu, mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania, Chaneta, Annie Kibira, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF), Michael Mwita.

No comments:

Post a Comment