Monday 8 May 2017

Bentick ndiye mshindi mbio za baiskeli Coco Beach

Na Mwandishi Wetu
JOHAN Bentick juzi aliibuka shujaa baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mashindano yam bio za baiskeli ya Coco Beach Tour.

Mshindi huyo alitumia dakika 23:55 kukamilisha kilometa 18, ambapo lilishirikisha washiriki mbalimbali kutoka jijini Dar es Salaam.

Wa pili katika mbio hizo za baiskeli alikuwa, Salum Kizoka aliyetumia dakika 26:20 huku Maulid Amani alimaliza watatu kwa dakika 26:20.

Washiriki walichuana kuanzia Mnazi Mmoja kupitia Palm Beach, Oysterbay, Yatch Club, Toure Drive hadi Coco Beach, ambako washindi walikabidhiwa zawadi zao.

Mshindi wa kwanza aliondoka n ash 250,000, wakati mshindi wa pili sh 150,000 na mshindi wa tatu alibeba sh 100,000 huku kila mshiriki akiondoka na cheti.

Mratibu wa shindano hilo Mbaraka Mbwambo alisema baada ya kuandaa mashindano hayo wako mbioni kuandaa mengine kulingana na kalenda watakayokuwa wameiandaa ambayo yatakuwa na muundo wa mashindano yasiyopungua nane(8) kwa mwaka.

Mashindano hayo yatakuwa katika maeneo manne, ambapo  mazingira yake wanajitahidi kuyaandaa  ratiba yake itakapokamilika wataitangaza.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli Tanzania (Chanbata), Godfrey Muhagama aliwapongeza waandaaji.

Pia aliwataka aliwataka viongozi wa Chama cha Baiskeli mkoa wa Dar es Salaam, wachezaji na wadau kujitahidi kuhamasisha ili mchezo huo uwe unafanyika mara kwa mara mkoani kwao.


Alisema mkoa unapofanya vizuri ndipo taifa linakuwa na nafasi kubwa ya kupata wachezaji wazuri watakaounda timu za taifa.

No comments:

Post a Comment