Tuesday, 30 May 2017

Geay, Huche wang'ara mbio Marekani, Ufaransa

Na Mwandishi Wetu
WANARIADHA wa Tanzania wameng’ara katika mbio mbalimbali za kimataifa nje ya nchi baada ya kushika nafasi ya kwanza na ya tatu.

Gabriel Geay alimaliza wa kwanza katika mbio za kimataifa za kilometa 10 za Marekani za Bolder Boulder kwa kutumia dakika 29:02:19 na kutwaa jumla ya dola za Marekani 8,000 (sawa na sh 17,904,000).

Mbio hizo za Marekani zilishirikisha zaidi ya wakimbiaji 50,000 kutoka duniani kote, huku kitimu, Tanzania ilishika nafasi ya nne.

Wanariadha wengine wa Tanzania walioshiriki mbio hizo na nafasi walizoshika ni pamoja na Ismail Juma (18) aliyetumia dakika 30:43:99 na Josephat Joshua (20) kwa dakika 30:58:17.

Wanariadha hao ndio walikuwa wakiunda timu ya Tanzania iliyoshika nafasi ya nne na kuondoka na dola za Marekani 6,000 wakati ushindi binafsi wa Geay umempatia dola 3,000 na pia amelamba bonasi ya dola 3,000 kutoka kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas.

Wachezaji hao watatu wakagawa zawadi ya dola 6,000, amapo kila mmoja ataondoka na dola za Marekani 2,000.

Kwa mujibu wa Katibu wa Riadha Tanzania (RT), wachezaji hao watarejea leo jijini Dar es Salaam na kukatisha ziara yao katika chuo kikii komoja cha Marekani baada ya Juma kuugua ghafla.

Aidha, mwanariadha mwingine wa Tanzania, Stephano Huche mwishoni mwa wiki aling’ara katika mbio za marathoin za Saint Michel zilizofanyika nchini Ufaransa baada ya kumaliza wa pili kwa kutumia saa 2:15:26.
Huche amefunzi kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya riadha yatakayofanyika London, Uingereza Agosti akiungana na akina Alphonce Felix, Said Makula, Fabian Joseph na Jaffer Ngimba.

1 comment:

  1. aisee napenda kuonana na stephano huche my wajina

    ReplyDelete