Saturday 12 December 2015

Riadha Tanzania yawapiga pingu waandaaji wa Ngorongoro Marathon



Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
RIADHA Tanzania (RT) imezisimamisha mbio za Serengeti kwa muda usiojulikana baada ya kuwepo ubabaishaji mkubwa wakati wa kuendesha mbio hizo mwaka huu imeelezwa.

Kaimu katibu Mkuu wa RT, Ombeni Zavalla alisema jana kuwa, hatua hiyo ilifikiwa baada ya kikao kilichofanyika katikati ya wiki hii kati ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), RT na waandaaji wa mbio hizo kujadili mapungufu yaliyojitokeza.

Zavalla alisema kuwa, wamezisimamisha mbio hizo baada ya kubaini mapungufu kibao yalijitokeza ikiwemo ubabaishaji katika zawadi, usimamizi na utawala, ambavyo navyo havikuwa sawa sawa.

Akifafanua mapungufu hayo, Zavalla alisema kwa upande wa zawadi waandaaji hao waliahidi kutoa sh.. milioni 1.5 kwa washindi wa kwanza na pili kwa wanawake na wanaume wakati washindi wa pili kila mmoa alitakiwa kupewa sh.milioni 1 na watatu sh. 500,000.

Lakini waandaaji hao walishindwa kutimiza ahadi hiyo kwa upande wa zawadi, ambapo washindi wote walipewa fedha pungufu tofauti na walivyoahidiwa.

Alisema pia waandaaji hao waliendesha mbio hizo bila ya kushirikiana na Chama cha Riadha cha Mkoa wa Simiyu, wanariadha walinusurika kugongwa na magari baada ya kutokuwepo kwa watu wa usalama na hakukuwa na wasimamizi wa kutosha na wenye uelewa wa mchezo huo.

Matatizo mengine yaliyoikeza ni pamoja na waandaaji wa mbio hizo kutosajiliwa na kuwashirikisha wanariadha kutoka nje ya nchi kama Kenya bila kuwaombea vibali RT.

Alisema ni kosa kubwa kwa waandaaji wa mbio kushirikisha wanariadha wa nje bila ya kuwaombea vibali kwa RT.

Aidha, BMT imeiagiza RT kukutana na waandaaji wote wa mbio hapa nchini na kuwapa mafunzo kuhusu taratibu zote za uandaaji wa mbio hizo ili kuepuka migogoro katika mbio wanazoandaa.

No comments:

Post a Comment