Wednesday 16 December 2015

Eto'o apewa nafasi ya kuifundisha timu ya Uturuki ya Antalyaspor



ANKARA, Uturuki
NAHODHA wazamani wa Cameroon Samuel Eto'o (pichani), ameteuliwa kuwa kocha wa muda wa timu ya Uturuki ya Antalyaspor.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, aliyejiunga na  klabu hiyo Juni kwa mkataba wa miaka mitatu, amepewa mechi tatu za majaribio.

Mchezaji huyo amechukua timu hiyo kutoka kwa Yusuf Simsek, ambaye mkataba wake umesitishwa kwa makubaliano ya pande mbili tangy Desemba 7.

Antalyaspor itafanya uamuzi wa ama kumpa mkataba sa kufumi Eto'o baada ya mapumziko ya majira ya baridi.

Eto'o ataonozwa na kusaidiwa na Mehmet Ugurlu, ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo, wakati Mcameroon huyo akipia hatua ya kwanza katika kazi yake hiyo ya uongozi.

Hatua hiyo haikutarajiwa kwa mchezaji huyo wazamani wa Barcelona, Inter Milan na Chelsea, ambaye amewahi kuihusisha na matukio kadhaa tata dhidi ya shirikisho la soka la nchi yake pamoja na wachezaji wenzake.

Mmoja kati ya wachezai wenzake wa kimataifa, Patrick M'boma, alikiri kuwa "alishtushwa na kitendo cha Eto'o kupewa haraka kazi hiyo ya uongozi.

Lakini alibainisha kuwa Eto'o, ambaye alicheza naye pamoa katika fainali mbili za Mataifa ya Afrika, alikuwa na mawazo ya muda mrefu kuhusu nafasi hiyo.

"Najua ilikuwa mipango yake kuwa kocha, aliniambia miaka mingi iliyopita, alisema M'boma.

"Lakini ninachoua hana uzoefu. Nategemea atakuwa kocha mzuri, lakini sijui.

No comments:

Post a Comment