Monday, 28 December 2015

Jose Mourinho anasubiri kibarua Manchester United kabla hajarudi Real MadridLONDON, England
KOCHA Jose Mourinho anajaribu kuzuia vishawishi vya kurejea haraka katika klabu yake ya zamani ya Real Madrid wakati akisikilizia hali inavyoendelea katika klabu ya Manchester United na kwingineko Ulaya kabla hajafanya maamuzi ya mwisho kuhusu kibarua chake kijacho.

Madrid, ambako Mourinho aliondoka mwaka 2013 na kurudi Chelsea, wameonesha nia ya kumrejesha kocha wao huyo wazamani kuchukua nafasi ya mpinzani wake wazamani Rafa Benitez.
Lakini Mourinho kwa sasa anaonekana kama hana mpango wa kurejea Madrid.

Pia familia ya Mourinho, mkewe Tami, mtoto wake wa kike Matilde na yule wa kiume Jose junior hawana hamu ya kurejea katika jiji hilo la Hispania,ambalo walikaa kwa zaidi ya mismu mitatu.

Kingine kinachomfanya kocha huyo Mreno kutokuwa na hamu ya kurejea Madrid ni ile hali ya kutoelewana na baadhi ya wachezaji lakini tangu atimuliwe na Chelsea, amekuwa katika mipango ta Madrid.

Kwa sasa iko katika nafasi ya tatu, ambapo Jumatano watacheza na Real Sociedad na Valencia ya Gary Neville wayakwaana nayo Jumapili kabla ya kuanza kwa mapumziko ya majira ya baridi.

Timu hiyo ilifunga mabao 10 walipocheza dhidi ya Rayo Vallecano katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga, na kufuatia na kipigo kutoka kwa Villarreal.

Kwa sasa, Mourinho anasubiri kuangalia mwenendo wa rafiki yake na bosi wake wazamani Louis van Gaal Man United, ambao leo waikabili Chelsea kwenye Uwanja wa Old Trafford. 

Kocha huyo Mreno alitumia wiki kadhaa zilizopita akivua samaki na marafiki zake katika pwani jirani na Setubal. Sasa amekwenda Ureno kwa ajili ya mapumziko na familia yake.

No comments:

Post a Comment