Tuesday 22 December 2015

Tamasha la 14 la michezo na utamaduni la Karatu lilivyong'ara mwaka huu



Na Cosmas Mlekani, Karatu
TAMASHA la 14 la Michezo na Utamaduni la Karatu lilimaliziki mwishoni mwa wiki, huku likifungwa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Omary Kwaanq.

Mbali na riadha, tamasha hilo ambalo hufanyika Desemba kila mwaka, linashirikisha michezo ya soka, mpira wa wavu, mbio za baiskeli na ngoma za utamaduni pamoja na kwaya.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Omary Kwaanq (kulia), akienda kuanzisha mbio za kilomita 10 za Karatu. Kushoto ni mratibu wa tamasha hilo la michezo, Meta Petro na nyuma ni rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Gulam Rashid.
Tamasha lengo kuu la tamasha hilo ni kuibua na kuendeleza vipaji kwa watoto na vijana wa Karatu na vitongoji vyake na Tanzania kwa ujumla ili kuwawezesha kutumia michezo hiyo kupata ajira.

Kwa hivi sasa michezo imekuwa ni ajira kubwa sana duniani, hivyo vijana wa Tanzania pia wanatakiwa kutumia fursa hizo kujipatia ajira kama wenzao wa nchi zingine kama Kenya, Ethiopia na hata nchi zilizoendelea kama Marekani, China na zingine.
 
Timu pia zilichuana katika mpira wa wavu katika tamasha hilo la Michezo la Karatu.
Tamasha hilo lilianzishwa miaka 14 iliyopita na bingwa wa dunia wazamani wa mbio za mita 1500 Filbert Bayi akiwa na lengo la kuibua vipaji katika mchezo wa riadha ili kupata nyota wengine wa mchezo huo hapa nchini, ambao watangara kimataifa kama alivyongara Bayi.

Kama inavyoeleweka kuwa maeneo hayo ya Karatu, Mbulu na kwingineko katika mikoa ya Arusha na Manyara kuna vipaji vingi vya wanariadha kama alivyo Bayi, lakini vinakosa watu wa kuviibua na kuviendeleza, hivyo Bayi kupitia Filbert Bayi Foundation (FBF), aliamua kuanzisha tamasha hilo.

Katibu wa Kamati ya Wanawake ya Kamati ya Olimpiki Tanzania, Nasra Juma akiigagua timu ya Karatu kabla ya kuanza kwa fainali dhidi ya Magereza.
Hatahivyo, miaka ilivyokwenda Bayi aliamua kuongeza baadhi ya michezo pamoja na vikundi vya utamaduni ili kuwaongezea vijana fursa ya kujiajiri.

Michezo iliyofuata baadae ni pamoja na soka, baiskeli, mpira wa wavu na mingine ambayo baadhi yao sasa haichezwi tena kama netiboli.

Nasra akikagua timu ya Magere, ambayo ilifungwa 3-0 katika fainali dhidi ya Karatu.
Kwa upande wa riadha mchezo huo umekuwa na msisimko wa aina yake, ambapo pia umeibua vipaji vya wanariadha wengi nyota ambao sasa wanatamba hata nje ya mipaka kama akina Fabian Joseph, Dickson Marwa, Alphonce Felix na wengineo.

Pia kwa upande wa utamaduni kumekuwa na vikundi kama vya Sangoma Mbulumbulu, ambavyo kwa njia moja au nyingine mbali na kueneza utamaduni pia hutoa ujumbe mahsusi kama ule wa gonjwa hatari la Ukimwi ili kutoa elimu kwa wananchi wa Karatu na vitongoji vyake.


 

Wachezaji wa timu ya Karatu wakishangilia kwa staili ya `Magufuli" (wakipiga pushapu baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Magereza katika mchezo wa fainali.

Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA), Muharami Mchume akikagua moja ya timu za wavu zilishiriki tamasha hilo la michezo la Karatu.




Sekretarieti ya tamasha la Karatu wakiwa kazini kwenye viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu.

Washindi wa kwanza wa baiskeli kwa upande wa wanawake ns wanaume wakiteta baada ya kumaliza mbio hizo za Karatu za kilomita 30 na 60 katika viwanja vya Mazingira Bora Karatu.
 


Usalama ulikuwa wa kutosha katika tamasha la Karatu, ambapo walikuwepo askari wa usalama barabarani, gari la wagonjwa na mgambo ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kwa mujibu wa taratibu za mashindano ya kimataifa.
Pikipiki ikiendeshwa na John Muingerza ikiongoza wanariadha wa mbio za kilomita 10.
Mwenyekiti wa Taasisi ya FBF, filbert Bayi (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Omary Kwaanq wa pili kutoka kushoto) na makamu mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (Tava), Muharami Mchume kabla ya uzinduzi wa mbio za kilomita 10.
Mary Naali akimaliza wa tatu katika mbio za kilomita tano za wanawake za tamasha la Michezo la Karatu nyuma ya Angelina na Failuna Abdi waliomaliza wa kwanza na pili.


No comments:

Post a Comment