Wednesday, 16 December 2015

TETESI: Zidane KUFUNDISHA REAL MADRID WAKATI Benitez AKIKARIBIA KUTIMULIWA
MADRID, Hispania
KLABU ya Real Madrid imemuweka tayari Zinedine Zidane kama mbadala wa Rafa Benitez, kwa mujibu wa L'Equipe.

Taarifa hiyo inadai kuwa rais wa Real Madrid Florentino Perez hana imani na Benitez, wakati ikimteua Zidane kama kocha mkuu kama aliyokuwa akifikiria.

Licha ya kuungwa mkono hadharani Novemba, nafasi ya Benitez imekuwa matatani tena baada ya Jumapili kupokea kichapo cha bao -0 kutoka kwa Villarreal na kuiacha klabu hiyo pointi tano nyuma ya mahasimu wao Barcelona na  Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment