Tuesday, 29 December 2015

Mabingwa Simba kuanza kampeni dhidi ya Jamhuri Kombe la Mapinduzi ZNZ
Na Mwandishi Wetu,Zanzibar
MABINGWA wa Tanzania Bara Yanga na washindi wa pili Azam FC wako katika kundi moja la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo na waandaaji wake.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mashindano hayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Jumamosi, Januari 2 kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Kwa mujibu wa Kamati ya Michuano hiyo, jumla ya jumla ya timu nane zinatarajia kushiriki na zumepangwa katika makundi mawili, huku mabingwa watetezi Simba wakipangwa kufungua dimba na Jamhuri ya Pemba.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa, kabla ya mchezo huo wa  ufunguzi, jioni kutakuwa na mchezo utakaozikutanisha timu za Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) dhidi ya Watoza Ushuru wa Uganda (URA).

Simba katika mchezo huo imepangwa katika Kundi A pamoja na timu za JKU, URA na Jamhuri.

Kwa upande wa mahasimu wao Yanga, wenyewe wako katika Kundi B pamoja na timu za Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro, Azam FC na Mafunzo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Sharifa Khamis ametaja viingilio vya michezo hiyo kuwa ni  Sh. 10,000,5,000, 3000 wakati Urusi ni Sh. 2,000 tu.

Simba walitwaa taji hilo mwaka jana kwenye Uwanja wa Amaan baada ya kuichapa Azam FC.
 

No comments:

Post a Comment