Thursday, 3 December 2015

Mwili wa Willie Chiwango kuhifadhiwa Lugalo, Mwananyamala au Amana
 
Taarifa za hivi hivi karibuni zinasema kuwa; Willie Chiwango alifariki dunia usiku wa jana saa 5:30 katika hospitali ya Masana iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu anayejulikana kwa jina la Stephen, Chiwango mwenye umri wa miaka 61, alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kichwa.

Alisema kuwa mahuti yalimkuta katika hospitalini hapo akifanyiwa vipimo zaidi ili kujua tatizo la mwandishi huyo ambaye chombo chake cha mwisho kukifanyia kazi ni Tanzania Standard Newspapers (upande wa Daily News upande wa michezo).

Alisema kuwa mwili wa Chiwango bado uko Masana na ndugu wanafanya mipango ili kwenda kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia mahiti cha hospitali ya Lugalo, Mwananyamala au Amana.

Alisema baada ya kuuhifadhi mwili wa mpendwa wao, ndugu watakutana kwa ajili ya mazungumzo ili kujua mazishi yatafanyika lini na wapi.

Marehemu Chiwango ameacha mke na watoto wawili.
Tulimpenda Chiwango, lakini Mungu Amempenda Zaidi!

No comments:

Post a Comment