Saturday 12 December 2015

RISALA YA KATIBU MKUU WA TOC KWENYE MKUTANO MKUU WA KAWAIDA TAREHE 12/12/2015.



TANZANIA OLYMPIC COMMITTEE (TOC)
KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA

RISALA YA KATIBU MKUU WA TOC KWENYE MKUTANO MKUU WA KAWAIDA TAREHE 12/12/2015.

Ndugu Gulam Rashid, Rais, Kamati ya Olimpiki Tanzania, Ndugu Viongozi wa Serikali, Bara na Zanzibar,

Ndugu Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TOC,
Ndugu Wajumbe wa Mkutano Mkuu 2015, Wageni Waalikwa,
Waandishi wa Vyombo vya Habari, Mabibi na Mabwana:

Ndugu Rais,kwanza napenda nikushukuru ukiwa kama mwenyeji waMkutanohuukuwamgenirasmikutufunguliaMkutanohuuwamwakawakawaidawaKamatiyaOlimpiki Tanzania.

Ndugu Rais, walioko mbele yako niviongozi wa vyama vya Taifa zaidi ya 40 kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wanaoongoza michezo Kitaifa.

Kwa heshima na taadhima, kwanza naomba kwaniaba ya Kamati ya Olimpiki Tanzania niwakaribishe rasmi kwenye Mkutano Mkuuhuuwamwaka 2015utakaoanzamudamfupikuanziasasabaadayaufunguziwako.

NduguWajumbe,MkutanoMkuuhuuambaoniwakawaidakikatiba, niwamuhimusananawapekeekwasababuunakamilisha mambo muhimu ya shughuli ambazo Kamati yenu imefanya kwa siku 365 zilizopita na kupanga kwakuthibitisha shughuli za TOC kwa siku zingine 365 zijazo.

Pia. Naomba nichukue nafasi kuwakaribisha wageni wetu wote waalikwa katika Mkutanohuu.Karibunisana.

Mhe.Rais,Mkutano unaofahari kuwa nawe kama mgenirasmi, jambo ambalo hatujazoea hasa ukiwa mwenyeji wa Mkutano huu.

NduguRaismwakahuuKamatiyaOlimpiki Tanzania imefanyashughulizakekamailivyokwenyeKalendaya 2015.

Moja ya shughuli hizo ni maandalizi ya timu yetu ya Vijana 4 (Ngumi na Riadha) iliyoshiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa Vijana mjini Apia, Samoa.

Shughuli zingine ni kati ya zile 17 zilizo katika Mipango ya Olimpiki Solidariti.

Ndugu Rais, Ushiriki wa wanamichezo wetu umepungua sana kutokana na aidha vyama/Mashirikisho kutokuwa na wanamichezo wenyevi wango.

Mwaka 2016 Michezoya Olimpiki inategemea kufanyika mjini Rio de Jeneiro, Brazil.Ushiriki wa Tanzania katika Michezo hiyo umekuwa na mtihani mkubwa kwa vyama/mashirikisho yetu ya michezo kutofikia viwango vinavyotakiwa. Mpakasasa ndugu wajumbe, ni Riadha Tanzania (RT) pekee ambayo wanariadha wawili (2) mpaka sasa wamefikia viwango.

Kati ya Vyama/Mashirikisho ya michezo ambayo yalipendekezwa kujiandaa kwa michezo ya Rio 2016 ni Riadha Tanzania na Kuogelea ambao wameshiriki michezo yao ya dunia yanayoandaliwa na mashirikisho yao ya Kimataifa. Michezo mingine (Ngumi na Judo) hawakuweza kushiriki michezo yao ya Kimataifa.

Pamoja na kuwepo kwa mashindano ya Kimataifa ambayo vyama hivyo vinaweza kujaribu kufikia viwango bado vyama/mashirikisho hayo hayakuweza kuwasilisha mipango yao kwa Serikali na TOC kwa wakati muafaka ilikuona namna ya kuwasaidia.

Ndugu Rais wewe ni shahidi, mara nyingi wananchi wametoa lawama kwa Kamati ya Olimpiki Tanzania wanamichezo wetu wanapokosa medali au ushindi katika mashindano ya Kimataifa.
 BilanchikuwekezakatikamichezoVyamanaMashirikishoyaMichezoyataendeleakubebeshwalawamazakutoandaatimumapemainavyopasa.

Ndugu Rais, wewe nishahidi, viwango vya michezo vimepanda duniani.

Nchi nyingi duniani kwasasa vyama/mashirikisho yao ya michezo vimewekeza kwenye vijana wa umri mdogo wa chini (12),  mdogo (15) na mdogo kati (17). Lakini tukiulizana hapa tulipo ni vyama vingapi ambavyo vina mipango hiyo?

Tumekuwa na ukame wawanamichezo vijana, wakakamavu, na wenye vipaji vizuri ambao vinaweza kuanzishwa na kuendelezwa kuliwakilisha Taifa letu kwenye michezo ya Taifa na Kimataifa.

Bado michezo haichezwi katika Shule zetu, kuwepo kwa Umitashumta na Umisseta siyo ufumbuzi wa kutatua ukame wa wachezaji wa umri niliotaja hapo juu kama hakuna mipango mahususi ya kuwaendeleza vipaji vinavyopatikana wakati wa michezo hiyo. Bila kufanya hivyo michezo hiyo itakuwa kama tamashatu.

Majirani zetu na dunia kwaujumla wanapata vijana chipukizi mashuleni nakuwafundisha/kuwaendeleza hadi kufikia ngazi ya Kimataifa na kuwakilisha mataifa yao. Katika michezo niliyoitaja. Ni mategemeo yetu sote Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itafanya mabadiliko makubwa katika tasnia hii ya michezo.

MwishonapendakutoashukraninyingikwabaadhiyaVyama/MashirikishoyetuyaMichezoyaTaifa (NSA/NSF) kwaushirikianowaliouonyeshakwamwakammojauliopita.

PianatoashukranikwaviongoziwamichezowaSerikalizetuzotembili Bara na Zanzibar kwaushirikianotuliokuwanaomudawote, halikadhalikaMashirikayaUmma, watubinafsi, namakampuni. UshirikianotulioupatakutokakwaoumesaidiasanaKamatiyaOlimpiki Tanzaniakutekelezawajibu wake. VilevileKamatiinatoashukranizakekwaOlimpikiSolidaritiambaokwakiasikikubwandiyoiliyosaidiakuendeshashughuliza TOC, ikiwapamojanakufanikishamkutanohuu.

Ahsanteni kwakunisikiliza.

No comments:

Post a Comment