Tuesday 22 December 2015

Pongezi za TOC kwa rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuendeleza michezo katika kipindi cha uongozi wake wa miaka 10




TANZANIA  OLYMPIC  COMMITTEE (TOC)
KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA
PONGEZI/SHUKRANI  ZA TOC KWA  RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUENDELEZA MICHEZO KATIKA MIAKA 10 YA UONGOZI WAKE

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) Juma Pinto akimkabidhi tuzo rais Jakaya Kikwete kabla hajastaafu hivi karibuni. Kushoto ni aliyekuwa Waziri wa Kazi, Utamaduni, Vijana na Mchezo Fenella Mukangara na mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi.
Napenda kuchukua nafasi hii kuushukuru uongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa kuandaa hafla ya kutoa tuzo kwa wanamichezo 10 bora waliofanya vizuri kwa kuiletea heshima  nchi yetu katika miaka 10 ya uongozi wa mwanamichezo mwenzetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na kutoa tuzo kwa Wanamichezo bora waliofanya vizuri miaka 10 iliyopita,  vile vile TASWA ilimtunuku tuzo Mhe Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wako katika michezo.

Mhe. Rais, wakati anazungumza na wanamichezo waliokusanyika katika ukumbi wa Mlimani hapo tarehe 12/10/2015 alisononeka kwa wanamichezo wa Tanzania kutofanya vizuri wakati wa miaka 10 ya uongozi wake pamoja na kuleta walimu katika baadhi ya vyama vya michezo.

Mafanikio hata katika maisha ya kawaida ni mapambano hali kadhalika hata kupata mafanikio katika michezo ni mapambano. Katika miaka ya 70-80 michezo ilikuwa ridhaa, lakini kuanzia miaka ya 90 hadi sasa michezo imekuwa biashara na ajira kubwa kwa wanamichezo.

Kwa mfumo huo wa michezo kuwa biashara na ajira kila moja angefikiria kwamba tungepaswa kuwa na wanamichezo wengi  kwa hiari yao kuchangamkia mazoezi ya hali ya juu ili nao waweze kuwa wawakilishi wazuri wa nchi yetu na kujipatia zawadi nono za fedha, lakini badala yake hali inazidi kuwa mbaya.

Hali hii inawezekana vile vile imesababishwa na hali ya ukata wa vyama vya michezo ambao hawana uwezo wa kutafuta vipaji huko walipo hasa Vijijini, Wilayani na Mikoani. Katika miaka ya 70-80,  Vyama vyetu vilikuwa vinapata ruzuku kutoka Serikalini kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ruzuku ambayo ilikuwa inawasaidia kuendesha ofisi na kuandaa Mashindano  kama ya Taifa ambayo wanamichezo wengi wanakusanyika na vyama husika kufanya uteuzi wa wachezaji bora wenye vipaji ambao huwaendeleza. Huo mfumo kwa sasa haupo kutokana na hali inayotamkwa na vyama vya michezo kama ukata na Serikali (BMT) kutokuwa na fedha.

Katika risala yake wakati wa tuzo kwa wanamichezo bora, Mhe. Rais alikiri bila kuwekeza tusitegemee kupata mafanikio, lakini nani awekeze, kwa haraka kwa tulio na uelewa mdogo ni Serikali ndiyo iwekeze kama nchi zingine duniani inavyofanya.

Mhe. Rais amefanya mengi kuinua michezo wakati wa uongozi wake. Naomba nitaje chache:

1.     WALIMU WA MICHEZO KUTOKA NJE
Aliweza kuwalipa mishahara walimu wa michezo kama mpira wa miguu, netiboli, ngumi na riadha(pamoja na walimu wa riadha kutokuwa wa viwango) kupitia mpago wa ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba. Kila moja wetu aliona jitihada zake,  na nakiri kwamba kwa namna moja au nyingine, vyama/mashirikisho ya michezo hawakutekeleza wajibu wao kutokana na hali ya ukata. Hata wanamichezo wetu hawakutambua na kuona michezo kama ajira.

Mhe. Rais anakiri mafanikio yana gharama, bila nchi kuwekeza hafikirii kama tutakuwa na mwelekeo mwema hasa kwa vijana wetu kufanya vizuri katika medani ya Kimataifa. Nchi nyingi zinazofanya vizuri katika michezo ya kimataifa  kwa asilimia kubwa wamewekeza katika michezo. Pamoja na WHVUM kutengewa bajeti ndogo ya michezo, bado suala la kuwekeza haliwezi kukwepeka kwa hali ya sasa ya michezo duniani.

2.     MICHEZO YA UMITASHUMTA/UMISSETA
Tutakukumbuka hasa pale Mhe Jakaya aliporejesha michezo ya Umitashumta na Umisseta  mwaka 2007 baada ya kusimama kwa zaidi ya miaka 9.

Binafsi naamini kilichotufikisha hapa tulipo leo ni pamoja na kutofundishwa kwa elimu ya viungo (PE) sambamba na kutokwepo walimu wa masomo hayo kwenye shule zetu na kusimama kwa michezo hiyo  na  Michezo ya Majeshi (BAMATA).

Michezo ya Umitashumta/Umisseta ndiyo ilikuwa kiwanda cha kuandaa wachezaji ambapo wanapofanya vizuri hupata ajira katika taasisi za Serikali (JWTZ, Polisi, Magereza, Jeshi la KujengaTaifa) lakini kwa sasa imekuwa tofauti kwani taasisi hizo haziajiri kama ilivyo huko nyuma kutokana na kutofanyika Michezo ya Majeshi (BAMATA) ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa.

Ni zaidi ya miaka 8 tangu aliporejesha michezo ya Umitashumta/Umisseta kwa nia na madhumuni yakupata vipaji vitakavyoendelezwa na kuwa na nafasi nzuri ya kutuwakilisha Kimataifa. Imekuwa vigumu kuendeleza  vipaji vinavyoonekana katika michezo hiyo kwani hakuna maandalizi yaliyofanywa kuwaendeleza  baada ya michezo hiyo kumalizika. Hata wale wanaomaliza masomo yao katika ngazi husika hawapati ajira kutokana na taasisi za Serikali nilizotaja kutokuwa na ajira rasmi kama ilivyo zamani. Mpaka sasa nishule chache za binafsi  na taasisi zimekuwa na  mpango wa kuwasajili katika shule zao wanafunzi wazuri wenye vipaji na baadhi yao kutoa elimu bure (Scholarships) na kuwaendeleza katika baadhi ya michezo:
a.      Shule ya Sekondari ya Alliance, Mwanza (Mpira wa Miguu na Riadha).
b.      Shule za Filbert Bayi, Mkuza, Kibaha Mkoa wa Pwani (Riadha na Netiboli)
c.       Shule ya Sekondari ya Lord Baden Powel, Bagamoyo (Mpira wa Miguu kwa Wanaume na  Wanawake,  Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu na Riadha).
d.      Shule ya Sekondari ya Winning Spirit,Arusha (Riadha)
e.      Shule ya Sekondari ya Makongo, Dar Es Salaam (Mpira wa Miguu, Netiboli Kikapu na Wavu).

Naomba niishauri Serikali (Wizara ya Elimu na Tamisemi) kuunda Kanda ili kila baada ya michezo ya Umitashumta na Umisseta wanamichezo wenye vipaji wawekwe katika shule zilizo katika Kanda zitakazoundwa wakiendelea na masomo hali kadhalika na kucheza kwa Wizara husika kupeleka wataalamu (coaches) katika Kanda husika. Kama hilo haliwezekani, basi shule binafsi na taasisi zisaidiwe ili ziweze kuimarisha zaidi mipango waliyonayo ya kuendeleza michezo

Bila kuwa na utaratibu na mipango mahsusi, michezo ya Umitashumta na Umisseta,  itakuwa kama tamasha tu.
3.     UWANJA WA TAIFA
Hakuna ubishi kwa ushiriki wake katika ujenzi wa uwanja wa Taifa wakati wa uongozi wa Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa kama Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mpaka alipochaguliwa kuwa Rais wa awamu ya nne na kumalizia kazi za ujenzi zilizobaki.

Uwanja wetu ni mzuri sana, lakini matumizi yake kwa mchezo wa riadha yamekuwa nadra sana kutokana na gharama kubwa ambayo wakati mwingine  Riadha Tanzania inashindwa kuchangia hasa inapotaka kufanya michezo ya Taifa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka.

4.     MAFANIKIO YA MICHEZO WAKATI WA UONGOZI WAKO.
Mhe.Jakata wakati wa uongozi wake wa miaka 10 kulikuwa na mafanikio ambayo hayaridhishi kwa nchi kama Tanzania yenye watu zaidi ya Milion 45, lakini kutokana na hali halisi niliyotaja hapo juu naomba nitaje mafanikio hayo kama ifuatavyo:


1.      Samson Ramadhani NYONYI, (Riadha):”Marathon”>Dhahabu: Michezo ya Jumuiya ya Madola, Melbourne, Australia 2006

2.      Fabian Joseph NAASI, (Riadha): Mita 10000>Shaba: Michezo ya Jumuiya ya Modola, Melbourne, Australia 2006

3.      Martin SULLE, (Riadha) Km 21.1>Medali ya Fedha>Michezo ya Afrika, Algiers, Algeria, 2007

4.      Timu ya Netiboli, (Netiboli)>Medali ya Fedha>Michezo ya Afrika, Maputo, Msumbiji, 2011

5.      Timu ya Netiboli (Netiboli)>Kushinda Kombe la Mataifa 6, Singapore, 2012

6.      Timu ya Netiboli (Netiboli>Nafasi ya Pili, Mashindano ya Africa, Dar Es Salaam, 2012

7.      Timu ya Mpira wa Miguu watoto wa Mitaani (Street Children World Cup)>Dhahabu, Mashindano Kombe la Dunia, Rio de Jeneiro, Brazil, 2014

8.      Timu ya Mpira wa Miguu-Vijana chini ya Miaka 15>Medali ya Fedha> Michezo ya Vijana Afrika, Gaborone, Botswana, 2014.

Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid akifungua mkutano mkuu Zanzibar Desemba 12 mwaka huu. Kushoto ni Katibu Mkuu Filbert Bayi na Mhazini Mkuu Charles Nyange.
5.     SHUGHULI ZA TOC
Wakati wa uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamati ya Olimpiki Tanzania imeweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa vyama vya michezo, baadhi ya hizo shughuli zilikuwa ni kuendesha mafunzo ya ufundi kwa walimu wa michezo kutoka Vyama/Mashirikisho ya michezo wanachama wa TOC kwa kuleta Wakufunzi kutoka nje ya nchi hali kadhalika na Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kwa viongozi wa Vyama/Mashirikisho ya Mikoa na Taifa kwa nyakati tofauti.

Kwa ujumla Walimu 523 (448/75) na viongozi 380 (304/76) waliweza kupata elimu ya kufundisha wachezaji kwa madaraja tofauti na uongozi na utawala bora.
(Orodha Nyongeza “A” na “B”imeambatanishwa).



HITIMISHO
Kwa niaba ya Kamati ya Olimpiki Tanzania na kwa niaba yangu napenda nichukue nafasi hii kumshukuru Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kutoa posho za kujikimu, mavazi ya taifa, vifaa vya mazoezi na mashindano timu zetu za Taifa zilizowahi kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola (Melbourne, Australia 2006, New Delhi, India 2010 na Glasgow, Scotland 2014) na Olimpiki (Beijing, China 2008, London, Uingereza 2012).

Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitamshukuru Mhe. Bernard Camillius Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ushirikiano na WHVUM kuwatafutia mazoezi ya nje (China, Ethiopia, Uturuki na New Zealand) kwa kutumia mpango wa Diplomasia ya Michezo (Sports Diplomacy) wanamichezo wetu kabla ya Michezo ya Jumuiya ya Madola, yaliyofanyika Glasgow, Scotland mwaka jana (2014).

Akiwa kama mwanamichezo nambari moja hata baada ya kustaafu bado wanamichezo wenzako tutahitaji ushauri wake katika maendeleo ya michezo katika
nchi yetu.

Mwisho kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Rais wa awamu ya tano (5) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu kwa kuchaguliwa kwa kishindo wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015, Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na Mawaziri wote kwa kuteuliwa kuongoza nchi yetu kwa miaka tano (5) ijayo kwa misingi ya “Hapa Kazi Tu”

Ni matumaini yetu wanamichezo kwamba viongozi hao wataitendea haki michezo kuanzia ngazi ya mashule hadi Kimataifa kwa viongozi watendaji kuwa makini (serious) kwenye maeneo yao.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi. Kulia ni rais Gulam Rashid na mhazini msaidizi, Zaidi.
Nawatakia Wanamichezo wote kila la kheri kwa mwaka 2016.


Filbert Bayi
KATIBU MKUU



NYONGEZA “A”
TANZANIA OLYMPIC COMMITTEE (TOC)
KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA

1.    MAFUNZO YA WALIMU WA MICHEZO 2006-2015
NA.

TAREHE
CHAMA/SHIRIKISHO
MAHALI
JINSIA
JUMLA




MME
MKE

1.
APR., 2006
MPIRA WA WAVU
TANGA
25
5
30
2.
AUG. 2006
TAEKWENDO
ARUSHA
30
4
34
3.
APR.  2007
MIELEKA
MOROGORO
21
3
24
4.
SEPT. 2007
MPIRA WA MIGUU
ZANZIBAR
25
-
25
5.
MEI. 2008
KUOGELEA
DAR ES SALAAM
25
5
30
6.
NOV-DEC. 2008
MPIRA WA MIKONO
DAR ES SALAAM
27
3
30
7.
MEI.   2009
TENISI
DAR ES SALAAM
21
-
21
8.
MAR. 2010
BAISKELI
ARUSHA
25
2
27
9.
NOV.  2010
RIADHA
DAR ES SALAAM
19
4
23
10.
JUL.    2011
MPIRA WA MEZA
DAR ES SALAAM
16
5
21
11.
NOV.  2011
JUDO
KIBAHA
32
-
32
12.
JAN.   2012
NGUMI
KIBAHA
23
2
25
13.
MEI.   2012
MPIRA WA MAGONGO
TANGA
20
2
22
14.
AUG.  2012
MPIRA WA KIKAPU
MOROGORO
18
11
29
15.
MEI.   2013
MPIRA WA WAVU
TANGA
27
8
35
16.
JUN-JUL. 2014
TAEKWENDO
ARUSHA
28
1
29
17.
OKT.  2014
MPIRA WA MIGUU
DAR ES SALAAM
29
3
32
18.
JUL-AUG. 2015
MPIRA WA MIKONO
KIBAHA
17
10
27
19.
AUG. 2015
MIELEKA
KIBAHA
20
7
27


JUMLA



448

75

523

Mwanariadha wazamani wa kimataifa wa Tanzania, Mwinga Mwanjala (kulia), akitoa mafunzo ya kutupa tufe kwa walimu wa shule za msingi nchini. Mafunzo hayo yalifanyika jjijini Dar es Salaam.
NYONGEZA “B”
TANZANIA OLYMPIC COMMITTEE (TOC)
KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA

1. MAFUNZO YA UONGOZI NA UTAWALA WA  MICHEZO 2006-2015
NA.
TAREHE
CHAMA/SHIRIKISHO
JINSIA
JUMLA


MKOA
TAIFA
MME
MKE








1
JAN. 2006

MOROGORO
19
4
23
2
MEI. 2006
DAR ES SALAAM

19
5
24
3
JUN. 2006
SONGEA

19
2
21
4
JUN. 2007

ZANZIBAR
20
3
23
5
JUL.  2007

DAR ES SALAAM
13
2
15
6
MEI. 2009
DAR ES SALAAM

17
5
22
7
OKT. 2009

ZANZIBAR
22
8
30
8
JUL.   2010
DAR ES SALAAM

17
6
23
9
AUG-SEPT. 2010
ZANZIBAR

25
5
30
10
AUG. 2012
ARUSHA

23
5
28
11
JUN. 2013
MBEYA

30
8
38
12
OKT. 2013
PEMBA

25
5
30
13
OKT. 2014
KILIMANJARO

14
6
20
14
NOV. 2014
ZANZIBAR

26
4
30
15
JUN.  2015
MTWARA

15
8
23

JUMLA


304
76
380



No comments:

Post a Comment