Wednesday 13 April 2016

Liverpool kuikaribisha Borussia Dortmund marudiano robo fainali ligi ya Ulaya kesho


Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp akimpongeza beki wake Alberto Moreno (katikati) wakati wa mchezo wa timu hiyo.

LONDON, England
TIMU ya Borussia Dortmund kesho itashuka kwenye Uwanja wa Anfield kucheza na wenyeji Liverpool katika mchezo wa marudiano wa robo fainali wa Ligi ya Ulaya.
 
Bao la ugenini la Divock Origi, ambalo baadae lilifutwa na lile la kichwa la Mats Hummels na kufanya mchezo kuwa sare ya 1-1 mjini Dortmund, liliiweka Liverpool katika nafasi nzuri wakati Jurgen Klopp akirudiana na klabu yake yazamani.
 
Hatahivyo, kocha wa Dortmund Thomas Tuchel ana uhakika timu yake inaweza kutinga nusu fainali licha ya Liverpool kuwa na rekodi nzuri dhidi ya mpinzani wake huyo wa Ujerumani, ambapo Liverpool haijafungwa katika mechi 15.

"Pia tunaweza kufunga mabao ugenini, na tunaweza kufunga zaidi ya bao moja, alisema Tuchel, ambaye timu yake imekata tamaa ya kuifukizia Bayern Munich katika Ligi Kuu ya Ujerumani ya Bundesliga baada ya mara mbili kukubali kurudishwa mabao yake na kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Schalke.

"Tulikuwa hauogopi. Tulipata nafasi kibao na kushinda, alingeza, huku Dortmund ikiwa haijafungwa katika mechi 13 tangu mwanzono mwa mwaka huu.

Kiungo wa Liverpool James Milner alisema kuwa watautumia vizuri uwanja wao wa Anfield wakisaka kutwaa taji la 12 Ulaya, matatu yakitoka katika michuano hii.

Ratiba Kamili:
Shakhtar Donetsk v Braga
Matokeo mchezo wa kwanza: 2-1

Sparta Prague v Villarreal

Mchezo wa kwanza: 1-2

Sevilla v Athletic Bilbao 

Mchezo wa kwanza: 2-1

Liverpool v Borussia Dortmund 

Mchezo wa kwanza: 1-1

No comments:

Post a Comment