Saturday 12 September 2015

Winchi laanguka Macca na kuua watu 107 waliokuwa wakisali leo



RIYADH, Saudi Arabia
SERIKALI ya Saudi Arabia imeanzisha uchunguzi ili kujua sababu za winchi (Crane)kuanguka katika mji mtakatifu wa Macca, na kuuwa watu 107.

Winchi kubwa lenye rangi nyekundu liliangukia sehemu ya msikitiki mkubwa uliokuwa umejaa waumini wakiendelea na ibada.
Taarifa zilisema kuwa upepo mkali na mvua kubwa ndio zilizosababisha winchi hiyo kuanguka.

Ilielezwa kuwa awali kulikuwa na taarifa kuhusu rekodi ya usalama katika eneo hilo la ujenzi la Saudi.

Msikiti huo mkubwa unaojulikana kama, Masjid al-Haram, ndio mkubwa zaidi duniani ambao unazunguka sehemu takatifu ya Waislamu, inayojulikana kama, the Kaaba.

Angalau watu 230 walijeruhiwa katika tukio hilo la aina yake. Haijafahamika watu wangapi wameumia wakati winchi hilo lilipoangukia msikiti huo.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:23 za jioni kwa saa za hapa jana Ijumaa.
Picha iliyopiga miezi miwili iliyopita kutoka katika minara ya Abraj al-Bait Towers ikionesha waumini wa Kiislamu wakisali katika msikiti mkubwa uliopo katika jiji takatifu la Macca. Winchi kadhaa zilianguka leo na kuua watu kadhaa
Picha za video zilizotumwa mtandaoni zinaonesha sehemu ikianguka, huku sauti za watu waliochanganyikiwa zikitoaka, miili na damu zikionekana katika sakafu ya eneo la msikiti huo.

Kiongozi wa mambo ya ndani ya nchi hiyo, Lt Sulayman Bin-Abdullah al-Amr, alisema uchunguzi unafanyika ili kujua madhara ya tukio hilo, na "usalama uliokuwepo katika maeneo haya.

Essam al-Ghalib, mwandishi wa Jeddah, alisema winchi hilo lilianguka na kuvunja kipande cha seminti chenye uzito mkubwa na kuwaagukia watu ambao ama walikuwa wakisali au kutembelea katika eneo hilo.

Mecca kwa sasa inajiandaa kupokea maujaji kwa ajili ya hija ya kila mwaka, ambapo hadi watu milioni mbili wanatarajiwa kuwasili katika jiji hilo la Saudi kutoka duniani kote mwezi huu.

Taarifa zingine zinasema kuwa msikiti huo mkubwa kwa sasa umezungukwa na winchi 15 kubwa kwa ajili ya kazi ya ukarabati inayoendelea katika eneo hilo.

"Saudi Arabia inatakiwa kufikiri tena kuhusu usalama wa hatua za usalama katika eneo hilo, alisema, ambapo eneo hilo lilikuwa na watu kama 800,000 katika msikiti wakati ajali hiyo inatokea.

No comments:

Post a Comment