Sunday, 6 September 2015

Gari la mashindano laacha njia na kuua sita wakiwemo wajawazito wawili
MADRID, Hispania
GARI la mashindano katika mbio za Hispania limeacha njia na kuvamia umati wa watu na kuwaua sita wakiwemo wajawazito wawili na mtoto wa miaka minane.

Pia katika ajali hiyo watu sita wamejeruhiwa vibaya na kwa sasa wamelazwa kutokana na majeraha.

Mashindano hayo yalifanyika katika Manispaa ya La Coruna iliyopo Kaskazini Magharibi mwa Hispania, ambapo dereva wa gari hilo alishindwa kulimudu gari hilo na kujikuta akiliachia liwavae watu.

Kwa watu ambao walishuhudia ajali hiyo walisema kuwa gari hilo liliruka na kuwavaa watu hao waliokuwa pembezoni mwa barabara.

Lilikuwa ni gari aina ya Peugeot 206 lenye nambari  39 ambalo lilikuwa kwenye mwendo wa kasi  na dereva wake amejeruhiwa.

Katika eneo hilo hakukuwa na alama za kuwaweka watu mbali zaidi na njia iliyokuwa ikitumiwa kwa magari hayo.

Waliokuwa kwenye gari hilo ni pamoja na dereva wake, Sergio Tabeayo Sande maarufu kama Tisi  akisaidiwa na Luis Prego Miguel.

Kwa sasa kutokana na ajali hiyo shindano hilo limefungiwa hadi hapo baadaye na pia Polisi imesema watu  16 wamelazwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha La Coruña wakipatiwa matibabu zaidi

No comments:

Post a Comment