Friday, 18 September 2015

Rais Mugabe asoma hutuba tofauti, wapinzani wahoji uwezo wake wa kuongozaHARARE, Zimbabwe
RAIS wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka 91 Robert Mugabe alisoma hotuba tofauti na ile aliyotakiwa kuisoma wakati akifungua bunge la nchi hiyo hivi karibuni, kosa ambalo liliwafanya wapinzani kuhoji uwezo wa kiakili wa kiongozi huyo mkongwe barani Afrika.

Mugabe, ambaye ni mtawala pekee aliyebaki kusini mwa Afrika ambaye alitawala nchi hiyo tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1980, alisoma hutuba ile ile aliyoitoa Agosti 25, akiiomba China kusaidia kufufua uchumi wa Zimbabwe.

Mugabe alimaliza hotuba hiyo bila hata ya kuingiliwa, ambapo msemaji wake aliwalaumu viongozi huku akiahidi kuwa rais huyo angeisoma tena hotuba hiyo katika siku ijayo.

"Mvurugano huo ulitokea katika ofisi ya sekretari. Hotuba hiyo aliyoisoma bungeni ilitakiwa kuwekwa kando, alisema msemaji huyo wa rais George Charamba.

Lakini chama kikuu cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC), ambacho kinakosowa utawala wake wa muda mrefu,alisema utata huo unasababisha kuhoji uwezo wake wa kuendelea kuongoza.

Wakati huohuo, siku moja baada ya kusoma hutuba hiyo kimakosa wakati wa ufunguzi wa bunge, wapinzani wameibuka na kulaumu hatua ya rais huyo kutorudi tena bungeni na kusoma hutuba sahihi.

Jumanne, Bwana Mugabe, 91, aliyewasili bungeni akiwa na gari lake la kipindi cha ukoloni la Rolls-Royce, alionekana kabisa kutokuwa na habari kuwa hutuba aliyoisoma kwa takribani dakika 20 ni ile aliyoisoma bungeni hapo mapema wiki tatu zilizopita wakati akilihutubia taifa.

No comments:

Post a Comment