Friday, 18 September 2015

Albino Kenya avamiwa na kukatwa viungo na watuhumiwa kutoroka


NAIROBI, Kenya
WAVAMIZI nchini Kenya walikata baadhi ya viungo vya mtu mwenye ulemavu wa ngozi ili kwenda kuviuza kwa wachawi, ambapo taarifa zilisema kuwa,  hatua hiyo imezua hofu ikihofiwa kuwa, huku ikidaiwa kuwa shambulio hilo limefanywa na watu kutoka nchi jirani ya Tanzania.

"Watu watatu walivamia nyumba yangu na kutaka pesa, alisema mtu huyo albino mwenye umri wa miaka 56 aliyejitambulisha kwa jina la Enock Jamenya, kutoka Magharibi ya Kenya katika wilaya ya Vihiga. "Nilipowaambia kuwa sina pesa, waliniomba sikio au mkono ili wakauze Tanzania.

Wavamizi hao walikata sikio, mkono, shingo na vidole, gazeti la Daily Nation liliripoti, lakini baadae watu hao walikimbia, wakimuacha Jamenya akiwa amepoteza fahamu na akiwa na majeraha kibao.

"Mmoja wa watoto wake alikuja asubuhi kumuangalia baba yake, ambapo alimkuta akiwa amelala chini katika dimbwi la damu,alisema kaka yake Nixon Muhole alipozungumza na gazeti la The Standard.

Katika nchi ya jirani ya Tanzania, baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakituhumiwa kununua sehemu ya viungo vya albino kwa ajili ya imani za kishirikina.

Vikundi vya haki za binadamu vimeonya kuwepo kwa hatari ya ongezeko uvamizi wa watu wenye ualbinism nchini Tanzania kutokana na kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

Mtunga sheria Isaac Mwaura, ambaye ana ualbinism, aliendelea kuonya kuwa wavamizi wamekuwa wakivamia Kenya kwa ajili ya kufanya biashara nchini Tanzania.

Karibu watu 76 wenye ualbino nchini Tanzania wameuawa tangu mwaka 2000, ambapo sehemu ta viungo vyao vimekuwa vikiuzwa karibu dola za Marekani 600 (euro 528) na ambapo mwili mzima unauzwa kiasi cha dola za Marekani 75,000, kwa mujibu wa wataalam wa Umoja wa Mataifa (UN).

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa watu kadhaa walionusurika wamebaki bilaya viungo vyao baada ya kukatwa na kuchukuliwa na wavamizi hao.

Vikundi vya haki za albino vilisema kuwa vinahofia wavamizi wanaweza kuilenga Kenya baada ya serikali ya Tanzania kutoa taarifa kali kwa umma kukomesha vitendo hivyo vya kikatili.

"Tunataka serikali kuchukua hatua kali kuhusu vitendo hivi, kwa sababu vinatiashia maisha yetu," alisema Martin Wanyonyi, kutoka taasisi ya kuwawezesha watu wenye Albinism.


No comments:

Post a Comment