Saturday, 12 September 2015

Mpigapicha mwanamke afunguliwa mashtaka kwa kuwapiga ngwala wakimbizi Hungary
BUDAPEST, Hungary
WAENDESHA MASHTAKA wa Hungary walisema kuwa watafungua uchunguzi wa jinai kwa kuvunja amani dhidi ya mpiga picha wakike aliyeonekana katika picha za video akimpiga teke mikimbizi aliyekuwa akikimbia kukwepa kizuizi cha pili.

Katika picha hiyo, ambayo imezagaa katika mmitandao mbalimbali duniani, Petra Laszlo anaonekana akimpiga ngwala mtu aliyekuwa amembeba mtoto wake, na akimpiga mtoto mwingine aliyekuwa akikimbia jirani na mji wa Roszke, jirani na mpaka wa Serbia.

Inadaiwa kuwa baadae Laszlo, aliyetimuliwa kutokana na vitendo vyake hivyo, alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Habari la N1TV, lenye maskani yake karibu na Hungary.

Vyama viwili vya upinzani vilifungua malalamiko dhidi ya Laszlo muda mfupi baada ya video hiyo kuanza kuoneshwa katika mitamdao ya kijamii Jumanne.
Mpigapicha mwanamke wa TV akimpiga ngwala mkimbizi aliyekuwa amembeba mtoto. Mpigapicha huyo ametimuliwa na kituo chake cha TV na uchunguzi unafanywa na waendesha mashtaka dhidi yake.

No comments:

Post a Comment