Sunday, 6 September 2015

Didier Drogba aanza kucheza soka Canada na kupiga hat-trickCHICAGO, Marekani
MCHEZAJI Drogba wa Montreal Impact ameifungia timu yake bao la hat trick katika ushindi wa 4-3 dhidi ya Chicago Fire katika Ligi Kuu Marekani.

Timu hiyo ya Chicago Fire ni timu ambayo alikuwa akitarajiwa kuitumikia mara baada ya kutoka Chelsea.

Drogba alijiunga na timu hiyo kuanzia Agost 22, lakini hakuichezea kutokana na kukabiliwa na majeraha.

Timu hiyo ilikuwa ikicheza vibaya na kujikuta ikiambulia kipigo cha mara kwa mara kutoka kwa timu za Canada hali iliyopelekea kocha wake Frank Klopas kufutwa kazi.

Lakini kwa sasa tangu kuanza kucheza Drogba ambaye huo mchezo wa ushindi ukiwa ni ndio mchezo wake wa kwanza ameanza kwa kufunga.

Ilikuwa ni dakika ya 27 ambapo Drogba aliifungia bao hilo la kwanza timu yake hiyo kufuatia pasi kutoka kwa Nigel Reo-Coker .

Timu ya Chicago Fire nayo ilisawazisha kupitia mchezaji wake Jeff Larentowicz aliefunga kwa penati iliyopatikana kutokana na madhambi aliyofanyiwa mchezaji wa timu hiyo Maxim Tissot.

Lakini Montreal iliongeza bao jingine kupitia mchezaji wake Wandrille Lefevre.

Chicago ilikuja kuongeza bao jingine kupitia mchezaji wake Gilberto ambae pia alikuja kuongeza jingine dakika 59.

Mnamo dakika ya 61 Drogba aliongeza bao jingine na kisha kuja kupiga shuti lililogongana na kipa Sean Johnson na kuanzisha bao moja.


No comments:

Post a Comment