Monday 10 September 2018

Mkurugenzi Mkuu TAA, Bosi JNIA Wawatembelea Wagonjwa

     Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela akimfuta machozi Bi. Nitisile Nzelya wakati akimfariji walipomtembelea juzi kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipolazwa akipatiwa matibabu ya kutolewa maji katika mapavu. Bi. Nitisile ni Msaidizi wa Ofisi kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
 Bi. Nitisile Nzelya (aliyelala kitandani), ambaye ni Msaidizi wa Ofisi kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akipokea msaada wa fedha kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela, alipomtembelea kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili juzi.
     Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa pili kulia) akiongozana na Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara, Bw. Pius Wankali (kushoto) kumjulia hali Mhandisi Umeme wa JNIA, Bw. Majaliwa Ngonji nyumbani kwake Majohe jijini Dar es Salaam baada ya kupata ajali eneo la Itigi mkoani Singida alipokuwa akienda Tabora kikazi hivi karibuni.

    Mtoto Sarah Paulo akimfurahisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela aliyempakata wakati alipokwenda nyumbani kwao maeneo ya Kivule kumsalimia Baba yake Mhandisi Umeme wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paulo Benjamin (mwenye fulana) aliyepata ajali ya gari eneo la Itigi mkoani Singida, wakati akielekea Tabora kikazi. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Paul Rwegasha (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara, Bw. Pius Wankali (kushoto).

No comments:

Post a Comment