Saturday 15 September 2018

Paul Pogba Amchanganya Mourinho


LONDON, England
KOCHA wa Manchester Uniteds, Jose Mourinho amesema hajui hatma ya kiungo wake nyota, Paul Pogba (Pichani), lakini amejipa moyo na kusisitiza kuwa, kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa bado ataendelea kuwepo katika kikosi hicho.
Hatma ya Pogba  Old Trafford  iko shakani tangu majira ya joto huku kukiwa na uvumi wa kuwindwa na klabu za Barcelona na Juventus.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia alisema mapema mwezi huu kuwa hakuna anayejua kitakachotokea kwa baadae na kocha wa Manchester United Jose Mourinho hana uhakika wa hatma ya kiungo huyo.
Kocha Jose Mourinho.
"Kwa wakati huu niko kizani," alisema Mourinho kuelekea mchezo wa jana dhidi ya Watford.
"Kitu kimoja kiko wazi sana kwangu katika siku zote hizi tuko pamoja hajawahi kuniambia anataka kuondoka.
"Paul  alijiunga na wenzake baada ya Kombe la Dunia wiki moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu, hivyo tuko pamoja kwa takribani miezi miwili sasa na hajaniambia kama anataka kuondoka au la.”
"Nina uhusiano wa moja kwa moja na wachezaji na hajaniambia kwamba  anataka kuondoka. Kama hajaniambia anataka kuondoka ni kwa sababu anataka kubaki."
Mourinho aliulizwa kama wakala wa Pogba  Mino Raiola  anajaribu kumshawishi kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 kuondoka, alisema hilo ni jambo jipya kwake.

No comments:

Post a Comment