Saturday 15 September 2018

Ivan Rakitic Bado Yupo Yupo Sana Barcelona


BARCELONA, Hispania
KIUNGO wa kimataifa wa Croatia, Ivan Rakitic amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain (PSG), lakini amesema hakuna anayeweza kumuondoa Barcelona.

Rakitic haoni hatma yake nje ya Barcelona pamoja na kuwindwa na klabu ya PSG.

PSG wamekuwa wakimuwania kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia, ambaye aling’ara na timu yake ya taifa kwenye fainali za Kombe la Dunia,  lakini Rakitic aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuondoka Barcelona.

Rakitic, ambaye alishinda La Liga na mataji matatu ya Ulaya katika msimu wake wa kwanza akiwa na Barcelona mwaka 2015, alitoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha kocha Ernest Vervede kushinda taji la La Liga msimu uliopita, anatazamiwa kuwa nahodha ajaye wa timu hiyo kufuatia kuondoka kwa kiungo Andres Iniesta na Javier Mascherano.

"Sioni pakwenda nikiondoka,” alisema Rakitic. “Kuna mada mbalimbali tumezungumza. Nilichukua siku kadhaa kufikiria na kugundua nilipo.

 “Sioni kitu chochote maalumu, najiona nina bahati. Naweza kucheza Barcelona, kuipigania beji hii na hicho kitu kikubwa. Pia mke wangu na mtoto wangu wa kike wanafuraha Barcelona.”

Rakitic  ameanza kwenye mechi zote tatu za La Liga, ambazo Barcelona imeshinda msimu huu na kuiwezesha klabu hiyo  kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.


No comments:

Post a Comment