BACELONA, Hispania
LIONEL Messi alifunga hat-trick yake ya 48 katika
historia ya soka wakati Barcelona ikiwasambaratisha mabingwa wa Uholanzi, PSV
Eindhoven kwa mabao 4-0 katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi wa Ligi
ya Mabingwa wa Ulaya.
Nahodha huyo wa Barca alianza mbio zake hizo za
kufunga mabao matatu katika mchezo huo pale alipofunga bao la kwanza kwa mpira
wa adhabu kabla shuti la Luis Suarez la umbali wa kama meta 20 kugonga mtambaa
panya.
Ousmane Dembele, ambaye yuko katika kiwango kizuri
cha uchezaji aliwatoka mabeki wawali na kuiwezesha Barcelona kupata bao lake la
pili akipiga mpira mkutoka nje ya boksi.
Messi alifunga bao la tatu baada ya kupata pasi pasi
ya juu kutoka kwa Ivan Rakitic kabla beki wa Barcelona, Samuel Umtiti kutolewa
nje baada ya kupewa kadi ya pili ya njano.
Licha ya kuwa 10 uwanjani, Barcelona walipata bao la
nne wakati Suarez hajampatia Messi mpira, ambaye aliupiga na kumpita kipa Jeroen
Zoet kutoka umbali wa kama meta 15.
Katika mchezo m,wingine wa Kundi B ulishuhudia Inter
Milan ikitoka nyuma na kuichapa Tottenham 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye
Uwanja wa San Siro.
Messi, ambaye sasa ni nahodha wa Barcelona baada ya
kuondoka kwa Andres Iniesta, anaonekana kuwa kuweka kando kufanya vibaya katika
Kombe la Dunia nchini Urusi, baada ya kufunga mara moja tu katika fainali hizo
katika hatua ya 16 bora.
Sasa mchezaji huyo amefunga mabao saba katika mechi
sita msimu huu, na alikaribia kufunga pale alipopiga mpira wa adhabu katika
kipindi cha pili na kutengeneza nfasi nzuri kwa Suarez na Roberto.
Mabao yake yote matatu yalikuwa mazuri. La kwanza
alifunga kwa mkwaju wa adhabu likiwa ni la nane kufunga kwa staili hiyo, baada
ya kupiga mpira uliojaa katika kona ya juu ya upande wa kulia wa lango.
Hadi sasa amefunga mabao 104, zikiwemo hat-trick nane
katika mashindano na amepachika mabao katika mechi mfululizo 14 za Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya, akifikia rekodi ya gwiji wa Real Madrid, Raul.
MWAKA
WA BACELONA?
Barcelona kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa
ikitolewa katika hatua ya robo fainali, huku maadui zao Real Madrid wakitwaa
taji hilo katika vipindi hivyo vyote.
Wachezaji wa Barca katika kipindi hiki cha majira ya
joto walizungumzia kuhusu umuhimu wa Ligi ya Mabingwa kwao wakati wakijaribu
kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015.
Msimu uliopita washindi hao wa mataji mawili wa
Hispania walionekana wako shapu dhidi ya wapinzani wao baada ya kushinda mechi
saba huko nyuma na alifunga mabao 13 katika mechi mbili huko nyuma, ingawa PSV
walikuwa wazuri zaidi tofauti na matokeo yalivyokuwa.
Wakianza na wachezaji tisa kati ya 11 waliocheza na
Roma msimu uliopita, Barceloma ilianza mchezo huo kwa nguvu huku Philippe
Coutinho, akiichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya, alipiga kichwa mpira wa krosi iliyochingwa na Suarez.
Zoet alifanya kazi kubwa kuokoa michomo ya wazi
kutoka kwa Sergi Roberto na Coutinho.
HISTORIA
YA MESSI
Barcelona imeshinda mechi 25 kati ya 27 zilizopita za
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya walizocheza kwenye uwanja wao wa Nou Camp, wakitoka
sare mbili. Na kwa mara ya mwisho walipoteza mchezo kwenye uwanja huo, Mei 2013
walipocheza dhidi ya Bayern Munich (3-0).
PSV Eindhoven haijashinda mechi zake tisa zilizopita
za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (wakitoka sare mara nne na kupoteza tano).
Messi amefunga katika mechi tofauti 30 za Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya, huku akipitwa na Raul (33) na Cristiano Ronaldo (32) wakifunga
dhidi ya wapinzani tofauti tofauti.
Amefunga mara nane kwa mikwaju ya adhabu mwaka huu.
Muangetina huyo amefunga hat-trick nyingi zaidi
kuliko mchezaji yeyote katika historia ya Kombe la Ulaya (8). Ameifungia
Barcelona hat-trick 42 na sita ameifungia timu yake ya taifa ya Argentina.
NINI
KIFUATACHO?
Barcelona itakuwa mgeni katika mchezo wa marudiano
utakaofanyika kwenye Uwanja wa Wembley wakati itakapokabiliana na Tottenham katika
mchezo wa raundi ijayo, huku PSV itakuwa mwenyeji wa Inter Milan – zote
zitafanyika Jumatano, Oktoba 3.
No comments:
Post a Comment