Monday 17 September 2018

KAMBI YA RIADHA YA DStv YAZINDULIWA MBULU



Makamu wa Pili wa Rais RT Ufundi, Dk Hamad Ndee (kulia), Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday (wa pili kushoto), mwanariadha waamani, Mzee John Stephen Akhwari (wa pili kulia) na  Mkuu wa Mawasiliano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana Mbulu mwishoni mwa wiki.

Ni katika maandalizi ya kuiletea Tanzania medali kwenye michezo ya kimataifa

Vijana 16 waanza kupikwa katika kambi hiyo maalum iliyopo Mbulu

•Wanariadha wakongwe wapongeza, Tanzania sasa kurejea kuwa kinara

MultiChoice Tanzania ikishirikiana na klabu yariadha ya Rift Valley ya Karatu imefungua kambi maalum ya raidha wilayan iMbulu ambapo wanariadha 16 watakuwa wakipati wa mafunzo kwa mwaka mzima.

Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na mwanariadha mwenye sifa ya kipekee duniani John Stephen Akhwari, katibu mkuu wa Shirikisho la RiadhaTanzania (RT), Wilhelm Gidabuday na Makamu wa Pili wa Rais wa RT (Ufundi), Dk. Hamad Ndee.

Kambi hiyo ina wanariadha wengi wenye umri mdogo, akiwemo Francis Damiano Damas, ambaye ni balozi maalum wa DStv na mshindi wa medali ya shaba katika mashindano ya vijana ya Jumuia ya Madola yaliyofanyika visiwa vya Bahamas mwaka jana.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa Mawasiliano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana, amesema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha kuwa riadha ina kuwa na mchango mkubwa katika kuliletea taifa sifa,  kutoa ajira kwa vijana wengi na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.
 
“Tunataka Tanzania ijulikane ulimwenguni kote kama chimbuko la mabingwa.Tumedhamiria kikamilifu kukuza mchezo huu na kufanya kama chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana wetu, lakini pia riadha ni mchezo, burudani na ni sekta nyeti kiuchumi kama ikiendelezwa.” 

“Tunataka kuusikia wimbo wetu wa  taifa katika mashindano makubwa ya riadha ya kimataifa, tunataka kuiona bendera yetu ikipepea juu katika kila mashindano makubwa ya riadha ya kimataifa ,tunataka mamia ya vijana wetu wenye uwezo mkubwa katika riadha washiriki kwenye mashindano makubwa, waweze kujipatia kipato na kuwachanzo cha maelfu ya ajira na hatimaye kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya nchiyetu,” amesema Mshana.
 
Kambi hii ilianza rasmi tarehe 1 Septemba 2018 na itasimamiwa na klabu ya Riadha ya Rift Valley kwa ufadhiliwa  Kampuni ya MultiChoice Tanzania, kwa mujibu wa makubaliano kati ya pande hizo mbili.

Kwa kuanzia kambi hiyo ina jumla ya  wanariadha 16 ambapo awamu ya kwanza ya mafunzo itakuwa kwa miezi mitatu (Septemba – Novemba 2018) na awamu ya pili (Januari- Machi 2019).
 
Kwa upande wake mgeni maalum katika ufunguzi huo na mwanariadha nguli aliyewahi kuweka rekodi ya aina yake Katika Michezo yya Olimpiki  1968 nchini Mexico, Mzee Stephen John Akhwari amesema kuwa huu ni uwekezaji mzuri uliofanywa na Kampuni ya Multchoice na ni mfano wa kuigwa na wengine.

"Ni kweli kabisa huu ni uwekezaji mkubwa na ni mfano wa kuigwa wa wngine, "amesema Mee Akhwari.

Naye Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday, amesema amefarijika sana na uwekezaji huo wa Multichoce.

Amesema Shirikisho la Riadha la Tanzania litahakikisha kuwa ufadhili huo unakuwa na manufaa na unazaa matunda yaliyotarajiwa ya kuleta medali nyingi zaidi katika mashindano ya kimataifa. “Ufadhili wa aina hii nimuhimu sana kwa maendeleo ya mchezo wa riadha .Tuna ahidi ushirikiano wetu wa dhati ilikufanikisha malengo na tutahakikisha kuwa tunatoa ushikiano unaostahili kwa wafadhili wetu,”amesema Gida.

Mwaka uliopita, kampuni ya MultiChoice Tanzania ilidhamini kambi ya riadha ya timu ya taifa na pia ilimdhamini mwanariadha Alphonce Felix Simbu, ambaye kwa sasa ni miongoni mwawanariadha tegemeo kwa nchi hii. 

Hivi sasa MultiChoice Tanzania inamdhamini mwanariadha kinda Francis Damiano Damasa mbaye ni mshindi wa medali ya shaba katika Micheo ya ya vijana ya Jumuia ya Madola iliyofanyika Bahamas mwaka jana.

No comments:

Post a Comment