Saturday 8 April 2017

Wanafunzi shule ya Filbert Bayi wakonga nyoyo wakati wa kukipokea Kifimbo cha malkia jijini Dar es Salaam leo



Wanafunzi wa shule ya msingi ya Filbert Bayi wakiwa katika picha ya pamoja na wakimbiza Kifimbo cha Malkia mara kilipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyererea (JNA) eneo la VIP leo.
Na Mwandishi Wetu

KIFIMBO cha Malkia wa Uingereza kimetua jijini Dar es Salaam leo huku wanafunzi wa shule ya Msini ya Filbert Bayi waking'ara na ngoma yao ya Mganda wakati wa kukipokea kifimbo hicho kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere  (JNIA).
Kifimbo hich kesho kitakimbizwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Ikulu, ambako litapokewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Wanafunzi hao wa shule ya Filbert Bayi walikonganyoyo za wakimbiza kifimbo hicho pamoja na wageni waalikwa waliofika uwanjani hapo kukipokea, ambapo walichenua kwa `atep zao bila kukosea, mbali na mavazi yao meupe na vitambaa vyekundu vichwani mwao.
Ndege ya Kenya Airways ndiyo iliyokibeba Kifimbo hicho kutoka Kenya na kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na watu mbalimbali wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Coke na Balozi wa Australia nchini Kenya, John Feakes.

Kifimbo hicho kilipotua nchini kilibebwa na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola Afrika, Gideon Sam pamoja na Rais wa TOC, Gulam Rashid na kuingia nacho katika jengo la kuwasilia na kuondokea abiria maarufu la VIP la JNIA.

 Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) leo. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Coke na Rais wa TOC, Gulan Rashid.
Akizungumza uwanjani hapo Sam alisema kuwa kifimbo hicho ni ishara ya kukaribia kufanyika kwa Michezo ya 21 ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Gold Coast, Australia Aprili mwakani.

Alisema kifimbo hicho kimetokea Kenya, ambao walikipokea kutoka nchini Nigeria.

Naye Feakes  alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuelimisha kuhusu kifimbo hicho, ambacho kinakimbizwa kila kabla ya michezo inayokuja ya Jumuiya ya Madola.

Rais wa TOC, Rashid alisema wanafurahi kukipokea kifimbo hicho , ambapo kesho watakikimbiza hadi Ikulu.

Bayi akitaja ratiba ya kifimbo hicho kesho asubuhi kitaanzia Azam TV kabla ya kwenda katika daraja la Nyerere na baadae kwenye Uwanja wa Taifa, ambako kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo za burudani kutoka African Stars `Twanga Pepeta’, JKT, Polisi na vikundi vingine, kabla ya kuanza mbio kwenda Ikulu.

Kifimbo hicho jioni kitakwenda Arusha katika shule ya St Judy na baadae kurudi jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Filbert Bayi wakicheza ngoma ya Mganda ya Manda mkoani Ruvuma wakati wa kukipokea Kifimbo cha Malkia ya Uingereza leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere, JNIA.
 

No comments:

Post a Comment