Wednesday, 3 June 2015

Kocha Rafael Benitez atua rasmi Real MadridMADRID, Hispania
KLABU ya Real Madrid imethibitisha kuwa, imemchukua Rafael Benitez kama kocha wao mpya kwa mktaba wa miaka mitatu.

Kocha huyo Mhispania mwenye uzoefu mkubwa katika soka alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba iliyoachwa wazi na Carlo Ancelotti wakati alipoachana na Real wiki iliyopita.

Kutangazwa kwa Benitez kumeiacha Napoli inayoshiriki Ligi ya Serie bila kocha baada ya Benitez kumalizana nao mwishoni mwa msimu na sasa atakuwa na kibarua cha kuiongoza Real kufanikiwa katika La liga na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Benitez ambaye ni kocha wazamani wa Real Madrid, aliiongoza Valencia kutwaa mataji mawili ya Hispania kabla ya kuifundisha Liverpool kwa miaka sita na kuiwezesha kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka 2005.

Kocha huyo alikwenda kuifundisha Inter na Chelsea, wakishinda mataji ya Ligi ya Ulaya na baadae aliiongoza Napoli kutwaa taji la Coppa Italia miezi 12 iliyopita katka kampeni yake ya kwanza kwenye uwanja wa Stadio San Paolo.

Real Madrid ilimaliza ya pili katika La Liga nyuma ya Barcelona msimu huu na kupoteza mchezo dhidi ya Juventus katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

No comments:

Post a Comment