Sunday, 21 June 2015

Man City yakubali kuilipa Liverpool pauni Mil 50 kumnunua SterlingMANCHESTER, England
KLABU ya Manchester City hadi sasa imewasilisha maombi mara mbili huku lile la mwisho likiwa linakaribia kiasi cha pauni Milioni 40. Yote yametupiliwa mbali na Liverpool.

Imebainishwa kuwa Liverpool hawataki kumuuza mchezaji wao Raheem Sterling mwenye umri wa miaka 20 chini ya kiasi cha pauni Milioni 50.

Chanzo kilichokaribu na klabu hiyo ya Merseyside imedokeza kuwa Man City haina mpango wa kukubali kumuachia mchezaji huyo endapo Man City hawataongeza pauni Milioni 10 ndipo wataweza kumuachia.

Man City pia wanajua kuwa klabu zingine kibao nazo zinamtaka mchezaji huyo ikiwemo Real Madrid ya Rafa Benitez, Arsenal na Chelsea.

Hawataki kabisa kumkosa Sterling na wanatarajia siku chache sijazo wanatarajia kuwasilisha ofa ambayo itawaridhisha Liverpool.

Man City pia wako tayari kuijaribu Arsenal kumnunua mwenzake na Sterling wanaecheza naye timu ya taifa ya England Jack Wilshere.

Hatahivyo, kocha wa Gunners Arsene Wenger anasisitiza kuwa shujaa huyo wa England aliyefunga mabao mawili wakati England ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Ulaya huko Slovenia Jumapili ya wiki iliyopita hauzwi.

No comments:

Post a Comment