Thursday, 11 June 2015

Ofisa Usalama wazamani China afungwa maisha kwa rushwa
BEIJING, China
OFISA Usalama wazamani wa China Zhou Yongkang amefungwa jela maisha ikiwa ni mwanasiasa mkubwa kabisa kushitakiwa kwa kosa la rushwa chini ya sheria ya Kikoministi.

Alipatikana na hatia ya rushwa, kukiuka taratibu na "kutoa siri za nchi nje ya nchi ", Shirika la Habari la China la Xinhua liliripoti.

Hadi anastaafu mwaka 2012, Zhou alikuwa mmoja wa watu wenye nguvu sana nchini China.

Na mwaka mmoja baadae alikuwa akichunguzwa kama mpango kabambe wa kupambana na rushwa wa rais Xi Jinping.

TV ya serikali ilionesha picha ya Zhou, 72, akikubali kosa katika shitaka lililoendeshwa `incamera kaskazini ya jiji la Tianjin.

Wakati akimjibu jaji, alisema hajakata rufaa.
"Nimebaini nimekiathiri chama na Watu wa China. Nakili na kujutia makosa," alisema.No comments:

Post a Comment