Sunday, 8 May 2016

Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzani Bara 2015-16 baada ya Simba kufungwa na Mwadui 1-0Na Mwandishi Wetu
YANGA leo imetetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2015/16 baada ya Simba kufungwa bao 1-0 na Mwadui ya Shinyanga katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 


Shamra shamra hizo za mashabiki wa Yanga ambao timu yao hataikucheza jana baada ya juzi kushinda dhidi ya Eseperaca ya Angola 2-0 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho, ziliendelea hadi nje ya Uwanja wa Taifa.

Kwa matokeo hayo, Simba yenye pointi 59 inaweza kufikisha pointi 68 sawa na Yanga endapo mabingwa hao watetezi watapoteza mechi zao zote tatu zilizobaki dhidi ya Mbeya City, Ndanda FC na Majimaji ya Songea zote ugenini.

Kutokana na mwenendo wa Simba, timu hiyo ina wakati mgumu kuifikia Yanga kwa pointi na kuizidi kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa kwani Yanga wana mabao mengi ya kufunga na kufungwa machache.

Kutokana na makali ya Yanga mechi hizo tatu zilizobaki ni ndoto kushindwa kupata sare hata moja tu ili kufikisha pointi 69, ambazo kamwe haziwezi kuguswa hata na Simba.

Bao lililowalaza Simba mapema jana na kumaliza matumaini ya angalau kuifikia Yanga, liliwekwa kimiani na Jamal Mnyate katika dakika ya 73 baada ya kumalizia pasi ya Kevin Sabato kufuatia mpira mrefu uliopigwa na kipa Jackson Abdulrahman.

Dakika ya 10 Haji Ugando wa Simba nusura afunge, lakini beki wa Mwadui Idd Mobby aliokoa wakati mpira ukielekea golini na kuutoa nje.

Mwadui ilipata pigo katika dakika ya 20 baada ya kipa wake Shabani Kado kutolewa nje baada ya kuumia na nafasi yake inachukuliwa na Jackson Abdulrazak.

Hamis Kizza alishindwa kutumia nafasi yake vizuri baada ya kupiga shuti katika dakika ya 31 na kutoka nje
Kiiza anapata nafasi nzuri ya kufunga katika dakika ya 65 lakini anashindwa kuujaza mpira wavuni.

Dakika tatu baadae Ajibu nusura aisawazishie Simba, lakini anashindwa kutumia vizuri nafasi aliyoipata na kuinyima timu yake bao.

 
Katika mchezo mwingine jana, Azam FC iliichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Mabao ya Azam yalifungwa na Kipre Tchetche na Himid Mao, wakati la Kagera lilipachikwa na Adam Kingwande.

Kwa matokeo hayo, Azam FC imeitoa Simba katika nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 60 na kuwaacha wekundu hao wa Msimbazi wakiwa na pointi zao 58.

Kikosi cha Simba; Justine Majabvi, Vicent Angban, Mohamed Hussein, Emery Nimuboma, Novalty Lugunga,,Juuko Murshid, Said Juma, Mwinyi Kazimoto, Peter Mwalyanzi/Brian  Majewega, Hamis Kizza/Mussa Mgosi na Haji Ugando/Ibrahim Ajibu.

Mwadui: Shaaban Kado/Jackson Abdulrahman dk20, Malika Ndeule, David Luhende, Iddy Mobby, Abdallah Mfuko, Jabir Aziz, Hassan Kabunda, Razack Khalfan, Kelvin Sabato/Salim Hamisi dk89, Rashid Mandawa/Julius Mrope dk69 na Jamal Mnyate.
 
MP W   D  L  GF  GA +/-  Points
27  21   1   64 16 48 68
28 17 9 2 44 22 22 60
27 18 4 5 43 15 28 58
28 13 8 7 31 20 11 47
27 10 12 5 24 22 2 42
28 11 7 10 28 26 2 40
28 11 4 13 26 28 -2 37
27 9 6 12 31 31 0 33
28 7 12 9 26 29 -3 33
27 9 6 12 20 36 -16 33
28 7 9 12 26 38 -12 30
28 7 8 13 29 41 -12 29
28 7 5 16 12 30 -18 26
28 6 7 15 19 33 -14 25
28 5 9 14 22 35 -13 24
29 5 7 17 16 39 -23 22
         

No comments:

Post a Comment