Wednesday 18 May 2016

Kocha Louis van Gaal akiri mashabiki Manchester United walitarajia mafanikio makubwa


Beki wa Manchester United, Chris Smalling (kushoto) akigombea mpira na mshambuliaji wa Bournemouth, Joshua King wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford jana. Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Mei 15, lakini uliahirishwa baada ya kutokea kwa tishio la bomu kwenye uwanja huo.

LONDON, England
KOCHA wa Manchester United Louis van Gaal anasema mashabiki wa timu hiyo walitarajia mambo makubwa kutoka katika klabu hiyo ya Old Trafford.

Man United iliifunga Bournemouth jana na kumaliza ya tano katika Ligi Kuu ya England, lakini mabingwa hao mara tatu wa Ulaya wamekosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa mara ya pili katika misimu miwili.

"Timu yetu iko katika mpito na na kama nilivyosema tangu mwanzo, alisema Van Gaal, ambaye alianza kuifundisha timu hiyo katika kipindi cha majira ya joto ya mwaka 2014.

"Labda nilihitajika kutuma ujumbe mzuri zaidi ya nilivyofanya.

Kocha wazamani wa Uholanzi Van Gaal alisaini mkataba wa miaka mitatu baada ya kuichukua timu hiyo miezi mitatu tangu alipotimuliwa David Moyes, ambaye aliitumikia timu hiyo miezi 10 akichukua nafasi ya kocha Sir Alex Ferguson.

Haijulikani kama Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 64 kama atashuhudia msimu wake wa mwishio Old Trafford, ingawa alisema kuwa anaamini ataendelea kuifundisha timu hiyo hadi atakapomaliza mkataba wake.

Baadhi ya mashabiki wa Man United wamemtaka kuondoka kocha huyo wazamani wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich kuondoka, wakati baadhi yao wakizomea katika mchezo wa mwisho wakishinikiza aondoke katika mchezo dhidi Bournemouth.

Van Gaal anaweza kuiongoza Man United kutwaa taji lake kubwa la kwanza tangu mwaka 2013 taji la Ligi Kuu ya England chini ya Ferguson wakati Jumamosi 
watakapokabiliana na Crystal Palace katika fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Wembley.

Lakini alikiri timu hiyo kumaliza katika nafasi ya tano ni sawa na hatua moja nyuma baada ya kuwaongoza Mashetani hao wekundu kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa katika msimu wake wa kwanza.
"Lengo letu katika mwaka wa kwanza na wa pili na watatu ni Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, alisema baada ya kushinda 3-1 dhidi ya Bournemouth.

"Ni kiwango cha juu na klabu kama Manchester United inatakiwa kucheza katika kiwango kama kile, lakini kuna klabu zaidi ambayo zinazotaka kucheza katika kiwango kile na hilo umeliona.

"Matarajio ni makubwa sana. Mashabiki wanatarajia mengi lakini nafikiri matarajio haya ni makubwa sana.

No comments:

Post a Comment