Tuesday 24 May 2016

Jose Mourinho afanya mazungumo na uongozi wa Manchester United kuchukua nafasi ya Van Gaal



MANCHESTER, England
KOCHA Jose Mourinho (pichani) anakutana na uongozi wa Manchester United leo kwa ajili ya mazungumzo kuwa mbadala wa Louis van Gaal kama kocha wa timu hiyo.

Van Gaal, 64, alitimuliwa Jumatatu, ikiwa ni siku mbili baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa taji la FA, kwa sababu ya kiwango kibovu cha tiu yake.

Man United ilimaliza ya tano katika msimamo wa Ligi kuu ya England msimu huu na ilitolewa katika hatua ya makundi ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Mourinho, 53, mmoja wa makocha aliyepata mafanikio makubwa katika soka, amekuwa hana kazi tangu Desemba baada ya kutimuliwa Chelsea.

Alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu katika vipindi vyake viwili alivyotua Stamford Bridge, na aliiongoza Porto na Inter Milan kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka 2004 na 2010.

Kocha hiyo Mreno pia aliiongoza Real Madrid kutwaa taji la Hispania mwaka 2012, na uteuzi wake utashuhudia muendelea wa upinzani na kocha wazamani wa Barcelona Pep Guardiola,ambaye ataanza kuifundisha Manchester City katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Kipa wazamani wa Man United Peter Schmeichel amempigia debe Mourinho, lakini alisema klabu itakubali uteuzi wake.

Mourinho alitimuliwa Chelsea baada ya kuanza vibaya utetezi wao wa taji la Ligi Kuu, ambapo walishindwa mechi tisa za kwanza kati ya 16.

Pia kocha huyo alijiingiza katika mgogoro mkubwa na daktari wa timu hiyo Eva Carneiro, ambaye alitimuliwa na alifungua kesi dhidi ya klabu hiyo akidai kunyanyaswa.

"Mourinho aligombana na mkurugenzi wa soka katika klabu hiyo, rais, daktari wa timu. Alifanya mambo tofauti na jinsi Manchester United wanataka klabu yao ya soka iendeshwe,alisema Schmeichel, 52.

No comments:

Post a Comment