Tuesday, 17 May 2016

Balozi wa Kili Challenge Mrisho Mpoto awaomba Watanzania kuchangia mfuko wa Ukimwi


Msanii wa Mashairi nchini, Mrisho Mpoto au Mjomba akizungumza wakati wa  ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Masuala ya Vijana uliofanyika jana kwenye hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam leo.

Na Mwabndishi Wetu
MUIMBAJI nguli wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto amesema kuwa atatumia kipaji chake cha uimbaji kutunga nyimbo za kupambana na unyanyapaa kwa watu wenye virusi vya Ukimwi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watu wenye ulemavu, Dk. Abdallah Possi akifungua mkutano wa mwaka wa masuala ya Vijana leo jijini Dar es Salaam.
Mpoto ambaye anajulikana sana kama Mjomba aliyasema hayo jana wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Masuala ya Vijana uliofanyika Ubingo Plaza jijini Dar es Salaam.

Mjomba alisema alizitaka taasisi na watu mbalimbali kuchangisha fedha kwa ajili ya kuzisaidia taasisi mbalimbali zinazoshiriki kusaidia waathirika wa Ukimwi.

Msanii huyo ambaye ni Balozi wa Kili Challenge,ambayo inahusika na kuchangisha fedha kupitia upandaji Mlima Kilimanjaro.

Alisema kuwa wafadhili kutoka nje ambao wanasaidia kuchangia mfuko huo wa kusaidia waathirika, siku moja wataacha kusaidia, hivyo aliwataka Watanzania kuchangia mfuko huo.

Alisema kuwa unyanyapaa ndio kimekuwa kitu hatari zaidi kwa jamii, hivyo aliwataka watu kuacha tabia ya kuwatenga wenye maambikizo na kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali.

Mjomba hivi karibuni aliteuliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Tume ya Kupambana na Ukimwi Tanzania (Tacaids) kuwa balozi wa Kili Challenge.

Witness Makanje (kulia) akitoa ushuhuda kuhusu kuishi na VVU na kufanyiwa vitendo vya unyanyapaa wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Masuala ya vijana leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Yussuf Mohamed naye wa Pasada akimsikiliza.
Akizungumza baada ya ufunguzi huo, msanii wa BongoFleva Banana Zorro alisema kuwa atajitahidi kuwaelimisha wapenzi wa muziki kuhusu madhara ya unyanyapaa.

Naye naibu waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Abadllah Posi alisema vijana wanatakiwa kujiepusha na madawa ya kulevya na pombi kwani ndivyo vyanzo vikubwa vya Ukimwi.
 
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Fatma Mrisho alisema vijana hasa wanawake ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa huo hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Fatma Mrisho akizungumza katika mkutano wa mwaka wa wadau wa vijana leo.
 

No comments:

Post a Comment