Wednesday 13 May 2015

Waziri Korea Kaskazini auawa kwa kusinzia mbele ya rais



SEOUL, Korea ya Kusini
Idara ya Ujasusi ya Korea ya Kusini imesema kuwa Waziri wa Ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.

Taarifa hiyo iliyotolewa bungeni imesema Hyon Yong-Chol alikutana na mauti yake baada ya kupigwa kwa kombora la kuangusha ndege mbele ya mamia ya maafisa wakuu serikalini mwishoni mwa mwezi uliopita.

Bw.Hyon inadaiwa kuwa alisinzia katika hafla iliyokuwa ikihutubiwa na rais Kim, jambo lililomuudhi sana kiongozi huyo wa kiimla na kuamua kuuawa kwake hadharani.

Hata hivyo ukweli wa ripoti hiyo haujabainika kutokana na usiri wa Serikali ya Korea Kaskazini.
Taarifa zingine zinadai kuwa, Waziri wa Ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.

Bw.Hyon alipandishwa cheo na kuwa Generali mwaka wa 2010 na kuuawa kwake kunatia shaka udhabiti wa uongozi wa rai Kim Jong -un.

Hyon alipandishwa cheo na kutangazwa kuwa waziri wa usalama wa taifa mwaka uliopita.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko Seoul anasema mauaji hayo ya kikatili mbele ya umma ikiwa yatathibitishwa, yanaonyesha athari za uasi dhidi ya Kim Jong-un.

Mapema idara hiyo ya ujasusi ilisema viongozi wakuu katika Serikali ya Korea Kaskazini wamekuwa wakiuawa kila mmoja kwa wiki.

Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa katika eneo la hadhara alikouawa.

Mara ya mwisho kwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kuamrisha kuuawa kwa kiongozi mkuu serikalini, ilikuwa mwaka 2013 alipoamuru aliyekuwa msaidizi wake Chang Song auawe
.
Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa katika eneo la hadhara alikouawa mbele ya umma.

No comments:

Post a Comment