Friday 8 May 2015

Mwanariadha India afa kwa sumu, wengine hoi hospitalini



NEW DELHI, India
POLISI wa nchini India wanachunguza kifo cha mwanariadha wakike mwenye umri wa miaka 15 na wengine watatu wakinusurika kifo baada ya kula kile kinachodaiwa matunda yaliyowekwa sumu, alisema waziri.

Ilielezwa kuwa wanariadha 10 walikula `othalanga matunda pori, ambayo yaliwekwa katika vifungashio vyenye sumu katika kituo hicho cha michezo huko Alappuzha kusini ya jimbo la Kerala kinachoendeshwa na Mamlaka ya Michezo India (SAI).

Wanariadha hao walikutwa wakiwa wamepoteza fahamu katika hosteli yaol Jumatano jioni na walikimbishwa hospitalini ambako mmoja wao alifariki dunia huku wengine watatu wakiwa katika hali mbaya.

Wote wanne inaaminika kuwa walisaini taarifa ya kifo, walisema viongozi hao, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu barua hiyo.

Walisema ni mapema mno kuhisi kuhusu kifo cha wanariadha hao chipukizi waliokuwa wakifanya mazoezi lakini ndugu wa waathirika hao walisema kuwa wasichana hao walikuwa wameathirika kiakili kutokana na kusumbuliwa na wanariadha wakubwa na makocha katika kituo hicho.

Waziri wa Vijana na Michezo Sarbananda Sonowal alisema polisi wanachunguza na Mkurugenzi Mkuu wa SAI alikuwa akiongoza taasisi hiyo pia.

"Sheria itachukua mkondo wake, lakini nakuhakikishia kuwa kama kuna mtu yoyote kutoka katika mamlaka ya michezo nchini India atapatikana na hatia kuhusiana na suala hili, atachukuliwa hatua za kisheria mara moja," alisema Sonowal katika taarifa yake.

Mkurugenzi Mkuu wa SAI Injeti Srinivas aliwaambia waandishi wa habari kuwa "ni tukio la kushtua sana ".

"Wasichana wanne walijaribu kujiua. Sasa tunataka kuwapatia vifaa vya bora vya afya, " alisema.

No comments:

Post a Comment