Sunday, 31 May 2015

Mwanasheria Kenya atoa ng'ombe, kondoo kumuoa binti wa ObamaNairobi, Kenya

MWANASHERIA wa Kenya ametoa kwa Rais Barack Obama ngombe 50 na vitu vingine vinavyohusiana na mifugo kwa ajili ya mahali ili kumuoa binti wa rais huyo Malia mwenye umri wa miaka 16, taarifa imeeleza.

Felix Kiprono alisema alikuwa yuko tayari kutoa ngombe 50, kondoo 70 nambuzi 30 ili kukamilisha ndoto yake ya kumuoa binti wa kwanza wa rais huyo kutoka taifa kubwa zaidi duniani.

"Tangu mwaka 2008 nilipata nia ya kumuoa Malia, " alisema, katika mahojiano na gazeti la Nairobi.

Wakati akipata nia hiyo, Rais Obama ndio kwanza alikuwa katika harakati za kutaka kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza huku Malia wakati huo akiwa na umri wa miaka 10.

"Ukweli ni kwamba, toka wakati huo sijawahi kutongoza msichana yeyote na niliahidi kuwa mwaminifu kwake. Nilishauriana haya na familia yangu na walisema wako tayari kunisaidia kuongeza mahali, " alisema.

Kiprono alisema anatarajia kumueleza Obama kuhusu suala hilo na ni matumaini yake kuwa, rais huyo atakwenda Kenya na binti yake huyo wakati mwezi ujao atakapoitembelea Kenya kwa mara ya kwanza tangu awe rais wan chi hiyo, nchi ambayo baba yake alikozaliwa.

Bibi yake Obama ambaye ni Mkenya, ambaye mapema miaka ya 90, bado anaishi huko Kogelo, magharibi ya Kenya, ambako kuna ndugu kibao wa rais huyo.

"Kwa sasa ninaandika barua kwa Obama nikiomuomba aongoxzane na Malia katika zira yake hiyo ya Kenya. Nategemea ubalozi utawasilisha barua hiyo kwa rais huyo," alisema.

Kiprono alikanusha kuwa anataka kumuoa binti huyo kwa lengo la kufuata utajiri.

"Watu huenda wakasema naenda katika familia hiyo kwa lengo la kufuata utajiri, pesa za familia hiyo, lakini hilo sio sababu. Nina mapenzi ya dhati, " alisisitiza.

Mwanasheria huyo kijana, ambaye umri wake haukuwekwa bayana, alisema tayari ameshapanga mipango yake ndoa hiyo itafungwa kimila,ambapo shampeni itakuwa ni maziwa ya mtindi, maarufu kama "mursik".

Kiprono alisema watakapoowa, yeye na binti huyo wa Obama wataishia maisha ya kawaida tu.

"Nitamfundisha Malia jinsi ya kukamua ngombe maziwa, kupika ugali na kuandaa vyakula vingine vya kiasili kama mwanamke yeyote mwingine wa Kalenjin woman," he said.

No comments:

Post a Comment