Wednesday 27 May 2015

Maofisa wa Fifa wakamatwa kwa tuhuma za rushwa



ZURICH, Uswisi
UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) utafanyika kesho kama kawaida licha ya kukamatwa kwa viongozi wake saba kwa sabbau ya madai ya kupokea rushwa ya dola za Marekani Milioni 150.

Miongoni mwa viongozi hao waliokamatwa jana asubuhi ni pamoja na makamu wa rais wa Fifa, Jeffrey Webb.

Uchunguzi wa tuhuma tofauti juu ya uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022 ulivyopatikana nao pia umeanza.

Lakini pamoja na tuhuma hizo lakini bado fifa imesisitiza kuwa, Urusi na Qatar bado zitaendelea kuandaa fainali hizo.

Sepp Blatter atakabiliana na Prince Ali bin al-Hussein katika uchaguzi huo wa kesho Ijumaa wakati akisaka kipindi cha tano cha kuongoza taasisi hiyo ya soka.

Viongozi saba wa Fifa walikamatwa jana baada ya Idara ya Haki ya Marekani ikitoa mashataka kadhaa dhidi ya viongozi hao kuhusu tuhuma za rushwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa serikali ya Uswis imesema kuwa maofisa hao walikuwa wakichunguzwa kuhusiana na tuhuma za kupokea rushwa ya mabilioni.

Taarifa hiyo ilisema kuwa walikamatwa na askari wa Uswisi kwa msaada ya Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI pamoja na Wizara ya Haki ya Marekani.

Pia ilisema kuwa maofisa hao tangu mwanzoni mwa miaka ya 1999 hadi sasa wameshachukua fedha ambazo ni sawa na dola za Marekani Milioni 100.

Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke alitembelea hoteli hiyo na kukagua lakini hata hivyo alishindwa kusema lolote kuhusiana na tuhuma hizo.

Lakini aliishia kusema kuwa tumeona taarifa hizi katika vyombo vya habari na kwa sasa tunajipanga kuja kutolea tamko.

Katika kamata kamata hiyo maofisa wa Polisi wakiwa wamevalia nguo za kiraia waliingia hoelini hapo na kisha kuchukua funguo na kwenda kwenye vyumba vya walipokuwa wamefikia maofisa hao wa FIFA na kuwakamata.

No comments:

Post a Comment